SYRIA:ANNAN APITISHA MKUTANO WA NGAZI ZA JUU


Mpatanishi wa Kimataifa kwenye mzozo wa Syria Kofi Annan amedhamiria kuitisha mkutano wa ngazi ya juu kuhusu nchi hiyo mjini Geneva  Jumamosi ijayo kwa lengo la kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu pendekezo alilowasilisha. 

Msaidizi wake Annan, Jean Marc Guehenno ametoa taarifa hiyo hii leo wakati akihutubia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva. 

Guehenno amesema kuwa Annan anafanya kazi na mataifa pamoja na pande zote zinazohusika kwenye mzozo wa Syria  ili kuleta amani na utulivu lakini muda unakimbia.