Hekari 15,000 zateketea na kusababisha hasara kwa wakazi wa kata tatu Wanging'ombeZAIDI ya Heka 15,000 za mashamba ya miti mkoani Njombe ‘sawa na viwanja 150 vya mpira ’ zimeteketea kwa moto katika kata za Makoga, Kipengele, na Igosi wilayani Wangingombe na kuwasababishia wananchi hao hasara ya mamilioni ya fedha kutokana na miti hiyo ya kupandwa.
Moto huu Ulizuka juzi majira ya mchana saa sita mchana na chanzo chake bado kikiwa ni kiulizo kwa wakazi hao kila mkazi akibuni chanzo chake ikiwa ni pamoja na utayarishaji wa mashamba na wachoma mkaa wahihisia kuwa ndio chanzo.
Atanasi Mwinuka, ni shuguda wa tukio hilo anasema kuwa moto huo ulianza kidogo kidogo na baadae kuenea eneo kubwa kutokana na nyasi kukauka na baadhi ya miti kuwa na asili ya mafuta na kuukuza moto huo.

Alisema kuwa moto huo umekuwa kukisababishw a mara nyingi na wanao andaa mashamba na kushindwa kuumudu na kuingia katika mapori ya miti ya kupandwa.

“Wachomba mkaa wamekuwa wakiusahau moto wanao tumia na kusababisha moto kuingia katika nyasi zilizo katika mashamba ya miti na kusababisha majanga kama haya,” alisema Mwinuka.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Njombe ilifika katika kijiji cha Mwilamba kata ya kipengele kwaajili ya kuuzima moto huolakini juhudi zikikwama kuumaliza moto huo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka analiagiza Jeshi la Polisi mkoani Njombe kuhakikisha kuwa chanzo cha moto huo kinatafutwa ili kudhibiti matukio ya moto.

“Jeshi la Polisi hakikisheni mnafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huu ili kudhibiti matukio kama haya ambayo huwatia hasara wananchi,” Alisema Sendeka

Pamoja na jeshi la polisi kutakiwa kufuatilia uchunguzi huo viongozi wa kisiasa na watendaji wametakiwa kuhakikisha kutoa elimu kwa wananchi kuto tumia uandaaji wa mashamba kwa kutumia moto.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Wangingombe, Ally Kasinge anasema kuwa katika wilaya anasema kuwa matukio hayo yamekuwa yakitokia mara kwa mara na chanzo kikibwa kikiwa ni wachoma mkaa na waandaaji wa mashamba.
Kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Njombe Deodatus Ndimbo anatoa tahadhari kwa wakazi wa mkoa wa Njombe kwaajili ya kuepuka majanga ya moto ambayo huwatia hasara, kwa kuto kumia moto uandaaji wa mashamba.


  • Tazama Video stori hii