Wafugaji kunufaika na benki ya kilimo Njombe


WAFUGAJI mkoani Njombe wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kucheleweshewa malipo yao kutoka kiwanda cha maziwa cha Njombe kutokana na mtaji wake kuwa ni mdogo na kuwasababishia kukwama kufanya baadhi ya shughuli zao.

Mfugaji wa ng’ombe wa Maziwa Aloisia Mdenye, jana alisema kuwa kutokana na mtaji mdogo malipo yamekuwa yakichelewa kutoka kiwandani.

"Malipo yamekuwa yakichelewa kutoka kiwandani kwa kuwa kiwanda chetu hakina mtaji wa kutosha lakini mtaji unge kuwa mkubwa malipo yengekuwa yanawahi," alisema Mdenye

Anayasema hayo alipotembelewa na Benki Kilimo iliyokuwa imeongozana na Maafisa wa kiwanda cha maziwa ambako ndio huuza maziwa yao na kusema kuwa pamoja na kuchelewa kwa malipo kiwanda hicho kimekuwa msaada kwao kwa kupokea maziwa yao yote.

Meneja kiwanda cha maziwa Njombe, Edwin Kidehele anasema kuwa wamepata Mkopo kutoka Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB Ambao utawezasha kuboresha mazingira ya uzalishaji wa maziwa kiwandani hapo.

Alisema kuwa wataongeza baadhi ya vifaa vya usafirishaji kwaajili ya kusambaza maziwa nje ya mkoa wa njombe, ikiwa ni pamoja na Majokofu, na magari maalumu ya kusafirishia maziwa.

Mshauri wa mifugo na afisa mifugo mkoa wa njombe Dr. George Katemba anasema kuwa wamekuwa na mradala wa mda mrefu na kiwanda hicho cha maziwa juu ya nini cha kufanyika kuboresha kiwanda hicho lakini upatikanaji wa fedha ndio ilikuwa kazi ngumu kufika muafaka.

"Tulikuwa kwenye mjadala mrefu juu ya wapi tutapata fedha kwaajili ya kuimarisha usindikaji wa maziwa kiwanda cha Njombe lakini tulipo sikia Benki ya kilimo inatoa mikopo tukashauriana tuombe na tukafanikiwa," alisema Dr. Katemba

Aidha Benki hiyo inaitembelea kiwandani hapo kwaajili ya kukagua wanaye mpa mkopo anastahili na kuzungukia maeneo mbalimbali kiwandani humo.

Mfuatiliaji wa mikopo wa Benki hiyo Dickson Pangamawe anasema kuwa serikali inamalengo ya kuwasaidia wakulima kupitia vikundi na kutoa ushauri wa kuimarisha shuguri zao za kilimo ili kuendana na masuala kauli ya viwanda.

Mjumbe wa bodi a Benki Rehema Twalib, hiyo anasema kuwa wameingia Njombe kuhakikisha kuwa wanatoa mkopo kwa kiwanda ambacho kinavigezo na kuangalia mahitaji yao kama ni kweli.

Meneja uzalishaji kiwandani hapo Kamtande Sikalwanda anasema kuwa wanamahitaji mengi ili kuongeza bei ya ununuzi wa maziwa kwa mfugaji.

alivitaja vitu ambavyo inapungua kiwandani hapo ni pamoja na Mashine za kuongezea thamani maziwa, vifaa vya kutunzia maziwa, na vingine vya kutengenezea jibini na kufanya maboresho ya baadhi ya mitambo am,bayo haijawahi kufanyiwa hivyo tangu kufungwa kwake wakati wa mradi wa kiwanda cha maziwa unafungwa.