WANAOENDESHA MAUAJI KIBITI WAUAWA NA POLISI

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.
Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata ya Ikwiriri, wilaya Rufiji Kanda Maalum ya Polisi Rufiji.
“Askari Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walianza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia askari kwa risasi, askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na hakuna atakaye baki.
Mkuu wa Operesheni Maalun za Jeshi la Polisi, Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas akiwa katika eneo la tukio akizungumzia namna Jeshi la Polisi lilivyofanikiwa kuuawa watu wawili awanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji watu katika Ikwiriri na kibiti. (Kushoto kwake ) ni Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi Rufiji, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga akiwa ameshika silaha aina ya Rifle 375 iliyokutwa katika eneo la tukio. Picha na Tamimu Adam.

from Blogger http://ift.tt/2vrJ3mU
via IFTTT