TUNDU LISSU APEWA MAKAZI MAPYA RUMANDE Y

Wakili wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kukamatwa kwa mteja wake kunaonyesha dhahiri kuwa na msukumo wa sababu za kisiasa kwani hakuna alilofanya na kwamba kinachodaiwa ni uchochezi hakina mashiko.
Akizungumza na waandishi wa habari jana usiku, Fatma Karume alisema kuwa licha ya Polisi kumaliza kumhoji kiongozi huyo lakini hawakumwambia kosa la uchochezi analodaiwa amelitenda ni lipi na alimchochea nani kufanya uhalifu.
Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kuelekea Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa wanasheria.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno alithibitisha kukamatwa kwa Mwanasheria huyo wa CHADEMA lakini hakuwa tayari kueleza sababu za kukamatwa kwake, akisema kuwa akifikishwa kwenye mamlaka husika watajua makosa yake.
Akifafanua maana ya uchochezi, Wakili Fatma Karume anayemtetea Tundu Lissu amesema kuwa, ni lazima uwe umemshawishi mtu kutenda jambo ambapo jambo hilo pia lazima liwe kosa vingine hakuna uchochezi hapo.
“Nimekwenda kumwakilisha mteja wangu Tundu Lissu Kituo Kikuu cha Polisi “Dar Es Salaam Central Police” jioni ya leo (jana Alhamisi). Anashikiliwa kwa makosa ya uchochezi kinyume na kifungu cha 390 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code). Nimewauliza Polisi wanadhani Tundu Lissu amemchochea nani na ni kosa gani la jinai ambalo mtu huyo aliyechochewa amelitenda. Jibu nililopokea ni Bado Tunachunguza.”
Fatma Karume akizungumza leo asubuhi na waandishi wa habari amesema kwa Jeshi la Polisi halijui ni lini litampeleka Tundu Lissu Mahakamani kwa sababu bado wanaendelea na uchunguzi.
Jambo hilo lilionekana kumshangaza sana wakili huyo ambapo alisema kwa uelewa wake, upelelezi unatakiwa kukamilika kwanza ndipo mtu akamatwe ambapo kwa wakati huo wanakuwa wapo tayari kumpeleka mahakamani.
Katika kuhakikisha haki ya mteja wake ya kufikishwa mahakamani inapatikana, wakili huyo alisema wamefungua maomba katika Mahakama Kuu ya Tanzania wakiiomba mahakama hiyo iliamuru Jeshi la Polisi limfikishe mahakamani Tundu Lissu kwani ameshahojiwa.
Kukamatwa kwa Tundu Lissu kumekuja ikiwa ni siku moja tangu alipokaa ndani ya ukumbi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa zaidi ya saa tatu akihofia kuwa atakamatwa na Polisi pindi akitoka nje.
Kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA, Polisi wameondoka na mtuhumiwa huyo kutoka Kituo Kikuu cha Polisi kwenda nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi.

from Blogger http://ift.tt/2uQ24Tk
via IFTTT