Jerry Muro Apigwa Chini Yanga

KATIBU Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, jana amemtambulisha rasmi, Dismas Ten kuwa Ofisa wa Habari wa klabu hiyo. Kabla ya utambulisho huo, Dismas alikuwa ofisa habari wa Mbeya City ya Mbeya ambayo pia inashiriki Ligi Kuu Bara kama Yanga.
Hii ina maana kuwa, Yanga haitakuwa tena na aliyekuwa ofisa wa habari wake, Jerry Muro ambaye hivi karibuni alimaliza kifungo chake cha kufungiwa mwaka mmoja alichopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Jerry alifungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, chini ya mwenyekiti
wake, Wakili Wilson Ogunde kwa kosa la kudharau uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkwasa alisema amemtambulisha Dismas baada ya ofisa huyo kumaliza mkataba wake wa miaka minne Mbeya City. “Nichukue nafasi hii kumtangaza
Dismas kuwa ndiye ofisa wetu wa habari mpya atakayefanya kazi pamoja na Chicharito (Godlisten).
“Hiyo yote ni katika kukiboresha kitengo chetu cha habari cha Yanga ili kifanye kazi yake vizuri ndani ya klabu yetu,” alisema Mkwasa.

from Blogger http://ift.tt/2tdw4YS
via IFTTT