UJERUMANI WAANZA VYEMA CONFEDARATION CUP.

Mabingwa wa soka wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani leo walikuwa uwanjani katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Confedaration Cup dhidi ya timu ya taifa ya Australia.
Mchezo huo ulikuwa wa piga nikupige ambapo Ujerumani walitangulia kupata bao la kwanza dakika ya 5 kupitia kwa Larsi Standi kabla ya Tom Rogic kuisawazishia Australia dakika ya 41 na dakika ya 45 Julian Draxler aliipatia Ujerumani bao lapili.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa Ujerumani kuongoza bao 2 kwa 1 na katika kipindi cha pili dakika ya 48 Leon Goreztka aliiandika Ujerumani bao la 3 kabla ya Tomi Juric kuipatia Australia bao la pili.
Kwa matokeo hayo Ujerumani wanakuwa sawa kwa point na Chile ambao jana waliifunga Cameroon huku Australia na Cameroon wenyewe wakibaki na alama sifuri.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rKRNqg
via IFTTT