RC ANNA MGHWIRA ‘AMKALIA KOONI’ MBUNGE WA HAI, FREEMAN MBOWE

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa za kuondoa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimanjaro Veggies si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji.
Image result for ANNA MGHWIRA
Mghwira alitoa kauli hiyo jana alipotembelea shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara ili kujionea hali ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika shamba hilo linalomilikiwa na Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
“Sheria iko wazi, inasema tusifanye shughuli zozote za kibinadamu zenye madhara kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kwa mujibu wa sheria na shughuli hii ina madhara makubwa kwa mazingira na hata kwa binadamu,” alisema Mghwira.
“Shughuli hii nzuri na ni uwekezaji mkubwa. Ninavyofahamu kilimo cha strawberry kikishatema maji lazima yaende mahali hata kama unatumia umwagiliaji wa kisasa wa matone. Maji yanakuwa na madhara kwa binadamu wanayoyatumia.”
Mghwira alisema kuwa licha ya mmiliki wa shamba hilo kukubaliana na mkuu wa wilaya kuwa amevunja sheria na angeondoa mazao yake ifikapo Mei 23 mwaka huu, hakufanya hivyo na badala yake alianza kulima mazao mapya.
Imeelezwa kuwa Mbowe alishawahi kuomba viongozi wa mkoa katika kikao cha RCC kuitishwa kikao ambacho kitajadali masuala ya mazingira na umuhimu wa kuheshimu umuhimu wa mazingira. Kikao hicho kilifanyika lakini RC akasema anashindwa kuelewa kwanini Mbowe ameshindwa kuheshimu.
Akizungumzia uharibifu huo, Mbowe alisema kuwa kwa sasa vijana zaidi ya 100 wamepoteza ajira lakini pia anajadiliana na wanasheria wake kuona nini kinafanyika kutokana na hatua hiyo aliyoiita ya uonevu wa serikali.
Chanzo: Mwananchi
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sSF6dh
via IFTTT