Showing posts with label June 21. Show all posts
Showing posts with label June 21. Show all posts
Spika Ndugai Afunguka Wapinzani Kususia Futari

Spika Ndugai Afunguka Wapinzani Kususia Futari

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameonyesha kuumizwa na kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kutojumuika pamoja na wabunge wenzao katika masuala ya kijamii ikiwepo kususia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kufuatia jambo hilo Ndugai amewaomba viongozi na wabunge kwa pamoja kuachana na mambo ya kujitenda kwani yanaweza kuleta athari kubwa ambazo hakuna anayehitaji, na kudai kama kuna mambo ambayo yanakwaza basi viongozi hao wanapaswa kukaa pamoja na kumaliza mambo hayo.
“Tumekuwa tukiandaa baadhi ya hizi shughuli siku ile ya bajeti tulipata nafasi ya kupata futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo, mabalozi tulihudhuria pale na ilikuwa imeandaliwa kwa wema kwa kweli. Leo (jana) pia na mimi nimepata nafasi ya kuandaa kama nilivyowataarifu lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema lakini ngoja nikiseme hapa kidogo, kuna baadhi yetu wengine wamekatazana rasmi kutohudhuria shughuli kama hizi, sasa mimi sitaki kuingilia uhuru wao, wana haki kufanya hivyo kama wanaona ni sawa lakini mimi mwenzao ningependa kuwashauri tu hasa viongozi wanaofanya mambo hayo kutazama tena njia zao, yako mambo mengine ni ya kijamii tu, ukifika mahali kiongozi unaanza kuwazuia watu hata mambo ya kijamii ujue unaenda mbali kidogo” alisema Ndugai
Spika wa Bunge aliendelea kutoa malalamiko yake dhidi ya vitendo vya baadhi ya wabunge wa upinzani kususia shughuli hizo za kijamii ambazo zinawaweka pamoja na kusema
“Hili bunge linavyoendeshwa labda wabunge wa kambi mbalimbali mnaweza msielewe bunge hili linaendeshwa katika mawasiliano mbalimbali ya sisi kwa sisi endapo kuna jambo linakwaza mpaka linasababisha hata watu wasipate futari kwa pamoja basi ni vizuri viongozi wa pande zote tukakaa tuzungumze na kuondoa vikwazo hivyo kama vipo maana mimi sijui kama vipo lakini kama havipo ni vizuri tuwe tunajumuika kwa pamoja, maana sera hizo zikienea na hakika kabisa na pande zingine nazo zitaanza na hakika matokeo yake italeta mipasuko ambayo hakuna anayehitaji hapa” alisisitiza Job Ndugai 
Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rVvKZf
via IFTTT


Mambo 11 Aliyoyapinga Baba wa Taifa Hayati Mwl. JK. Nyerere

Mambo 11 Aliyoyapinga Baba wa Taifa Hayati Mwl. JK. Nyerere

Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961.
Mwalimu Nyerere alizaliwa April 13, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria.
Alikuwa ni mototo wa chifu Burito Nyerere wa kabila dogo la wazanaki
Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi (kwa saa za Afrika Mashariki), katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.
Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani.
Mambo 11 aliyoyapinga baba wa taifa.
1. Ujinga
2. Ubinafsi Na Ufisadi
3. Ubepari
4. Ukabila Na Usehemu
5. Ubinafsishaji Holela Wa Mali Za Umma
6. Kuongozwa Kwa Rimoti Na Nchi Matajiri
7. Ubabe Na Vitisho Katika Uongozi
8. Umangimeza Na Ukiritimba
9. Usiri Wa Mikataba Na Makampuni Ya Kigeni
10. Rushwa
11. Uchu Wa Madaraka
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rVBC4r
via IFTTT


Ukiona Haya, Fahamu Muda wa Kubadilisha Betri la Simu yako Umefika!

Ukiona Haya, Fahamu Muda wa Kubadilisha Betri la Simu yako Umefika!

Ingawa betri la simu limetengenezwa na uwezo wa kuchajiwa mara kwa mara ila inafika muda ambao lazima libadilishwe tuu. Hasa inategemea utumiaji na utunzaji wa betri husika ila mara nyingi betri linaweza kuwa zima kabisa kati ya miezi 6 hadi miaka miwili ya kutumiwa.
Haya ndiyo ya kuangalia ili kutambua muda wa kubadilisha betri lako.
1.Muda wa betri kukaa na chaji umepungua na ata zaidi ya nusu ya mwanzo
Itakapofika muda ambao kiwango cha kupoteza chaji kimepungua kufikia hadi nusu au chini zaidi ukilinganisha na mwanzoni ulipoinunua kwa mara ya kwanza basi ujue haifai tena.
Muda mwingine utakuta simu inaonesha inakiwango cha asilimia nyingi tuu ya chaji alafu ghafla unashtukia imezima, ukiwasha inasema ‘battery low’, badilisha tuu betri.
Betri lisilofanya kazi kwa ufanisi linaathiri ata vitu vingine kwenye simu yako.
2. Simu inapata joto sana
Je unasikia simu inakuwa yamoto sana hasa hasa joto hilo likitokea eneo la betri? Epuka hatari, badili betri mara moja. Pia mara nyingi ikitokea hivi kwa simu utagundua pia ata betri halikai na chaji sana ukilinganisha na zamani.
3. Linachukua muda mrefu zaidi kujaa
Betri linatakiwa kuchukua masaa machache tuu kujaa, mara nyingi kwa simu za kisasa ni kati ya dakika 30 hadi masaa mawili hivi.
Ukiona kuna tofauti ya masaa kadhaa ukilinganisha na lilivyokuwa zamani basi ujue tayari ndani mwake mambo hayaposawa na hivyo uanze maandalizi ya kununua jipya kuepusha usumbufu wa kuchaji kwa muda mrefu kitu ambacho ni hatari.
4. Umbo limebadilika: Kuvimba
Hili jambo maarufu kwa watu wengi. Betri zuri si kwa simu ata bali ata kwenye magari, ni betri ambalo pande zote zimenyooka.
Kuonesha uvimbe katika pande yeyote ni dalili ya kwamba betri limeshachoka…yaani limetumika sana au limewekwa katika mazingira mabovu. Ukiona hivi ufanye haraka kununua jipya kwani betri lililovimba huwa na hatari ya kupata milipuko.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sW5oe7
via IFTTT


Walimu wa Vyuo Marekani Waruhusiwa Kubeba Bunduki Wakiwa Chuoniโ€ฆ.Kisa Hichi Hapa

Walimu wa Vyuo Marekani Waruhusiwa Kubeba Bunduki Wakiwa Chuoni….Kisa Hichi Hapa

Walimu wanapewa mafunzo ya kubeba bunduki wakiwa shuleni katika jimbo la Colorado nchini Marekani ili kuwalinda watoto kama hatua baada ya mauaji ya watoto mwaka 2012.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanayohusu bunduki na ya kutoa matibabu yalianza siku ya Jumanne katika kaunti ya Weld..
Watu 17 ambao watapewa bunduki hizo tayari wameshiriki mafunzo hayo.
Mpango huo ni wa kuruhusu watu wa kujitolea kuingia shuleni wakiwa na bunduki chini ya sheria ya Marekani ya kubeba bunduki.
Walimu walipelekwa kwa majiribio ya kupiga risasi karibu na Denver ambapo walijaribiwa uwezo wao wa kutumi bunduki.
Lakini hatua hiyo imekasirisha makundi kama ya Safe Campus Colorado, ambayo yanawashauri wafuasi kushinikiza mamlaka kusaidia kuondoa bunduki shuleni

from Blogger http://ift.tt/2sBshRl
via IFTTT


Kategori

Kategori