Mimi Nachukia Wezi..Kiama Chao Kimewadia Sasa – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema anachukizwa na baadhi ya viongozi wa Tanzania ambao wanatumia rasilimali za taifa kwa kuziiba kwa ajili ya manufaa yao huku akiahidi kuwa kiama chao sasa kimewadia.
Rais Magufuli amesema changamoto zilizopo nchini Tanzania kwa sasa zimeletwa na baadhi ya viongozi walioweka tamaa mbele na kwa sasa ni lazima wachukuliwe hatua ili nchi irudi kwenye mstari.
“Kuna changamoto nyingine zilisababishwa na viongozi wachache waliokuwa na tamaa za hovyohovyo, wakatufikisha hapa nataka niwahakikishie, nitalala nao mbele kwa kumtanguliza Mungu,“amesema Rais Magufuli huku akiendelea kuwaonya watu wanaoiba rasilimali za taifa kwa maslahi binafsi
“Tanzania hii ni nchi ya pili duniani baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vingi, lakini watu ni masikini, Huu umasikini hatukupewa na Mungu, Mungu alitupa utajiri lakini wachache wakatuuza, mimi nachukia wezi, na kwa kweli wezi watakoma tu,“amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli yupo mkoani Pwani kwa ziara ya siku tatu ambako anatarajiwa kuzindua viwanda vitano ambavyo ni Kiwanda vya vifungashio (Global Packaging Co Ltd), Kiwanda cha Matrekta (Ursus TAMCO Co ltd), Kiwanda cha Chuma (Kiluwa Steel Group), Kiwanda cha kukausha matunda na kiwanda cha vinyaji baridi cha (Sayona Fruits).
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sOtneH
via IFTTT