MESSI AMSIFU CRISTIANO RONALDO

Staa wa soka wa timu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kwamba huwa anapenda jinsi mashabiki wa soka duniani pamoja na vyombo vya habari vinavyowalinganisha (Messi na Ronaldo). Ronaldo ametupia magoli 16 katika mechi 10 za mwisho ambapo Real Madrid waliweza kutwa taji la ubingwa wa ligi kuu wa Hispania (La Liga) kwa msimu wa pili mfululizo na kushinda kombe la ligi ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo pia.
“Hapana, mara zote nimekuwa nikisema hili, kwamba [Ronaldo] kwa upande wake – anang’ara zaidi kwa uwepo wetu sote,” kituo cha ESPN kilimkariri Messi as akiiambia Tencent.
“Sisi sote tunajituma ili tupate matokeo mazuri kwa timu zetu, na linalosemwa nje ya hayo sidhani kama ni muhimu sana. Ronaldo ni mchezaji bora mwenye kiwango cha juu sana,” amesema Messi.
“Dunia nzima inajua, na ndiyo sababu yeye ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa duniani. Kila msimu mpya unapoanza, mchezaji unatakiwa kuwa bora kuliko msimu uliopita. Tunacheza ili tupate matokeo mazuri, tushinde mataji zaidi na kuingia kwenye fainali ya klabu bingwa Ulaya na pia kushinda ubingwa wa La Liga.”
“Mwaka huu haukuwa wetu. Tulijaribu kwa uwezo wetu wote, lakini ikashindikana; tukaishia kwenye kombe la Mfalme. Tunategemea msimu unaokuja utakuwa mzuri kwetu kwa maana ya kushinda mataji,” alimalizia Messi.

from Blogger http://ift.tt/2sTlyo6
via IFTTT