Lulu Diva Haambiliki Kwenye Vinguo Vifupi

MWANAMUZIKI aliyewahi kuwa video vixen Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa kwenye suala zima la mavazi haambiwi kitu kuhusu nguo fupi maana anazipenda kupindukia kutokana na kumtoa vizuri na kumfanya aonekane katika muonekano ‘amaizing’.
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Lulu Diva aliendelea kusema kuwa mara kwa mara amekuwa akikutana na watu ambao ni rafi ki zake ama watu anaoanzisha nao uhusiano na kumtaka asivae nguo fupi lakini suala hilo linashindikana kwa sababu asipovaa nguo hizo hajisikii huru na kuona kuna kitu kapungukiwa mwilini mwake.
“Kiukweli napenda sana kuvaa nguo fupi, tena ziwe zinabana uwii ndiyo zinanikosha mno, yaani huniambii kitu mtu akitaka tukosane aniambie nisivae nguo za aina hiyo. Kwa upande wa nguo ndefu kwangu hazina nafasi kabisa maana sijawahi kuvaa nikapendeza,” alisema Lulu Diva
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2soY7T0
via IFTTT