Siku mbili baada ya Azam kutangaza kumsajili mshambuliaji Mbaraka Yusuph, uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar alikotokea mchezaji huyo umeibuka na kupinga usajili huo, huku ukipanga kupeleka madai yake TFF.Kagera Sugar inapinga usajili huo kwa madai kuwa bado mchezaji huyo ana mkataba na wakata miwa hao wa Kagera.
Mbaraka ambaye amefunga mabao 12 katika msimu uliomalizika wa ligi, amekuwa akiwaniwa pia na Yanga, huku Kagera wakitaka kumbakiza mikononi mwao, lakini Azam wamefanikiwa kunasa saini yake kwa mkataba wa miaka miwili.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2riCo0c
via IFTTT