Baada ya Ushindi wa Jana..Wenger Aaanza Kuchonga..Atoa Kejeli Hili kwa Maashabiki wa Man United,Liver na Man City..!!!

.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameibuka na kuanza tambo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Middlesbrough juzi.
Mabao kutoka kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil yalitosha kuwapa pointi tatu Gunners katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Riverside. Pia, kipindi cha pili Alvaro Negredo aliipatia timu yake bao.
Ushindi huo umewapa nguvu mpya kwenye mbio za kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu England inayoelekea ukingoni.
Timu hiyo imebakiza pointi saba ili kuipiku Manchester City inayoshika nafasi ya nne. Hata hivyo kikosi hicho cha Guardiola kina michezo mingi ukilinganisha na Arsenal yenye mchezo mmoja mkononi.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amekiri, awali walianza kupoteza mwelekeo baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Crystal Palace wiki iliyopita.
“Nilihisi kwamba tulikuwa na mipango. Kama mlivyoona hatukucheza kwa kujiamini lakini kiuhalisia tulihitaji ushindi,” alizungumza Wenger wakati akihojiwa na Sky Sport.

from Blogger http://ift.tt/2pw2k6z
via IFTTT