MADAWATI YANATOSHEREZA NJOMBE

MKUU wa Mkoa wa Njombe DR. Rehema Nchimbi amewaagiza wakurugenzi kutoa maeneo kwa waalimu kwaajili ya kila shule kuwa na miti ya mipatachichi ili kuwapunguzia waalimu ukali wa maisha huku waalim hao wakimpatia pesa kwaajili ya madawati ikiwa ni kuunga mkono juhudi ya Rais ya kuhakikisha kuwa watoto hawakai chini.

DR. Nchimbi amewataka waalimu hao kuomba maeneo kwa wakurugezi wa halmashauri ili waalimu hao kupanda miti ya miparachichi na kusema kuwa katika shule zake hakuna wanafuzi wanao kaa chini na kusema kuwa halmashauri pekee ya Ludewa ndio kunashida ya madawati licha ya kuwa vifaa vyote vinavyo hitajika kuwepo.


Mkuu wa mkoa huyo amewaambia waalimu hao kuwa wajikite katika ujasiliamali na kujikwamua na ugumu wa maisha huku pesa walizotoa kwaajili ya madawati zilizotolewa na CWT kitengo cha wanawake na walemavu kurejeshwa kwao.


Walimu hao wamesema kuwa wanaunga mkono juhudi za Rais Dr. John Magufuli, kuhakikisha wanafunzi hawakai chini kwa kuchangia shilingi laki saba kwaajili ya kununua madawati.



Waalimu kitengo cha wanawake na walemavu mkoa wa Njombe wapo katika semina ya kujengeana uwezo na mafunzo ya ujasiliamali ili kujikwamua na matumizi mabaya ya pesa za mishahara.