Madiwani walalamikia kuwapo kwa Rushwa ya maandazi kutoka kwa mamalishe Makambako

MADIWANI wa halmashauri ya mji makambako mkoani Njombe wametakiwa kutoa elimu kwa wananchi ili kuacha tabia ya kuuza ardhi na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima kutokea katika ameneo yao.


Hayo yamebainisha na Bathoromeo Mwelange afisa tarafa ya Makambako kwa niaba ya mkuu wa wilaya Njombe katika kikao cha robo ya mwaka cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.

Mwelange alisema ushirikishwaji ukiwepo kati ya viongozi na wananchi migogoro inaweza kutatuliwa mapema pasipo kuleta madhara

Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiuza Ardhi kwa kazi kwa wageni kitu ambacho kisipo tiliwa maanani kunaweza kukatokea shida ya ardhi kwa wazawa wa maeneo ya kata zao.

“Ardhi inauzwa bila mpangilio huko vijijini kitu kinacho weza kuleta mtafaruku hapo baadae kwa kuwa watoto wao wanao wazaa sasa walioko shule watashindwa mahara pa kujenga na maeneo ya kulima chakula hayata kuwepo na kutakuwa na wageni wengi kuliko wenyeji, madiwani toeni elimu kwa wananchi wenu wapunguze kasi ya kuuza Ardhi,” alisema Mwelange.

Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Chesco Mfikwa aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kukemea vitendo viovu ikiwemo tabia ya kutoa na kupokea rushwa.

Alisema kuwa Rushwa imetawaliwa katika kila sehemu ya mji huo ambapo kumekuwa na wananchi wanao pokea rushwa na kutoa wote wanatena kosa.

“Kumekuwa na shida kwa migamo wa mji ambao wanapokea rushwa kwa mama Lishe na kuendesha maisha yao ya kupokea rushwa madiwani hakikisheni vitendo hivyo haviendelei, mamalishe hakikisheni mnadai lisiti kwa kila azabu mnayo pewa na afisa yoyote wa serikali,” alisema Mfikwa.


Hata hivyo baadhi ya madiwani walisema kuwa wamekuwa wakishihudia wananchi wakitoa rushwa ya chai na maandazi kwa Migambo hasa wanapo enda kuwakamata kutokana na Uchafu.

Diwani Baraka Kivambe diwani wa kata wa magegere alisema kuwa migambo wamekuwa wakipokea rushwa ya chai na maandazi asubuhi wanapo mamalishe, huku akusema kuwa wagaguzi wa nyama wamekuwa wakihongwa kilo za nyama wanapo enda kukagua nyama katika machinjia ya Makambako.

Aidha Diwani wa kata ya Mizani Perepetua Ngongi alisema kuwa kumekuwa na shida ya migambo kupokea rushw akwa madereva bajaji na kuweka bajaji zao mahara palipo katazwa na kuwa halmashauri iliweka azimio la kuwatoza faini madereva hao lakini kuwekuwa na uendelezwaji wa vitendo hivyo.

Aidha madiwani hao waliiomba serikali ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa makambako kuwawajibisha watendaji wabadhirifu kufuatia kudhoofisha mwenendo wa ukusanyaji mapato ya serikali ya halmashauri yao.