4G LTE YA TIGO SASA TANGA

Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Kanda ya
Pwani,.Goodluck Charles akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi    uliofanyika jijini Tanga leo kushoto kwake ni Benedict Mponzi ambaye
ni Meneja wa Biashara wa 4GLTE .
Katibu Msaidizi wa Klabu ya
Waandishi wa Habari mkoani Tanga(Tanga Press Club) Dege Masoli(L)
akipokea Kadi ya 4GLTE toka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za
Mikononi za Tigo Kanda ya Pwani,Goodluck Charles wakati wa uzinduzi wa
upatikanaji wa teknologia ya 4GLTE jijini Tanga leo.



Ni baada ya kuanza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi jijini Dar es Salaam 

Tanga, Novemba 25 2015. Wateja wa Tigo waishio Tanga sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkurugenzi wa kanda ya Pwani, Goodluck Charles.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Tanga, Charles amesema: "ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."
Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao. 
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Tanga kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti yenye kasi zaidi,” Charles amesema. Tanga ni moja wapo ya miji mikubwa Tanzania, na pia inajivunia bandari ndani ya Afrika Mashariki na kwa sababu ya bahari ya Hindi ni kivutio cha utalii nchini.
Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi  elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasí.

Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G itaanza kupatikana hivi karibuni kuwa ni Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza na Arusha, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufikisha huduma ya 4G katika kila kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Charles ameongeza kusema.

                          Imeandaliwa na :http://bongodailyupdates.blogspot.com/