Mgombea Ubungea apokea kwa masikitiko kifo Cha mwenyekiti wa Chama hicho




MGOMBEA  wa DP jombo la Njombe kusini ameelezea kusikitika kwake kuhusiana na kifo cha Mwenyekiti wa Chamachake Taifa Mch. Christopher Mtikila kilicho tokea alfajiri ya leo mkoani Pwani akitokea mkoani Njombe Kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa jimbo la Njombe Kusini.

Mgombea hiyo Jimbo la Njombe Kusini William Myegeta (Pichani wa kwanza kushoto), amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo na kuwa Chama kimepoteza kwa masikitiko makubwa sana na kuwa hata taifa pia limepoteza mtu huhimu sana kisiasa.

Alisema kuwa msiba huo ni mkubwa na kuwa kutokea kwa msiba huo ni mipango ya Mungu na kuwa alikuwa na lengo kubwa na Jimbo lake la Njombe Kusini na kuwa wangejua na inekuwa ni mipango ya Kibinadamu basi wangeweza kuzuia msiba huo.

"Kwa kweli msiba huu ni pigo kwa taifa zima na ni msiba mkubwa na taifa limepoteza mtu muhimi sana katika siasa kwani alikuwa ni mtetezi wa ukombozi wa watanzania," alisema Mgombea huyo.

Alisema kuwa hiyo ni mipango ya mungu na hakuna ambaye angeweza kuizuia ajali hiyo.

Aliongea kuwa kuhusu ratiba za msiba huo kwa kuwa ni wa kitaifa alisema kuwa ratiba bado haijatoka na itatoka hivi itakapo kuwa tayari.