Mch. Mtikila azikwa nyumbani kwao Milo leo jioni



SAFARI ya mwisho ya mwenyekiti wa chama cha DP taifa Marehemu Mch. Christopher Mtikila umeangwa leo kijijini kwao katika kijiji cha Milo kata ya Milo wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali wakiongoza na msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.

Ndugu na jamaa wa Marehemu mch. Mtikila wameelezea hisia zao juu ya kifo cha mchungaji huyo na kuwa Taifa limepoteza mtu supavu na asiye na woga katika kupigania haki za watanzania na mwanasiasa mkonge ambaye hakuwahi kukata tama kutokana na ujasili wake.

Akizungumza katika msiba huo uliokuwa umejaa simazi kwa wanasiasa Mutungi alisema kuwa wamefika kumsindikiza marehemu bila kuwa na itikadi ya chama chochote alisema kuwa Marehemu alikuwa ni kiongozi wa kitaifa wa chama hicho na kuwa alikuwa ni kiongozi shupavu na anautambua umuhumu wake.


Amesema kuwa watanzania kumeezi Mch. Mtikila ni kufanya yale aliyo kuwa anataka kuyafanya yanatimia na kuwa hakuwa mwoga kufuatilia jambo ambalo anaamini kuwa ni la kweli.


Amesema kuwa Mch. Mtikila alikuwa anatetea haki na kuwa aliwaomba watanzania kudumisha amani hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi, na kuwa amani tuliyo nayo hapa ncini ulimwengu mzima unautambua na unatamani.

Aidha kwa upande wa Dada Velonika Mtikila alisema kuwa msiba huu umepokelewa kwa masikitiko makubwa kwa ni ulitokea Ghafla.

Aidha kwa upande wake mmoja wa watu aliosoma nao, Petro Haule  alisema kuwa mchungaji alikuwa na misimamo tangu akiwa shuleni na kuwa aliendelea misimamo hiyo.