Hotuba ya Mzee Kingunge akiongea na waandishi wa habari alipotangaza kujiondoa CCM


Nilijiunga TANU na ni miongoni mwa wa anzilishi japo sikuwa miongoni mwa wale 17 wa kwanza. Hata hivyo wanachama wa awali waliobaki sidhani kama kuna zaidi ya Abdul Sykes na.mimi.
Mwalimu Nyerere aliniweka jaribu sana hasa kwenye masuala ya  mawazo.
Tulijenga TANU na AFRO vikiwa vyombo vya kupigania ukombozi wa mtanganyika na mzanzibari na bara la Afrika.
CCM iliridhi hayo na mimi nikiwa mwanzilishi miongozi mwa wale wa mwanzo.
Tuliijenga CCM kimuundo na kifikra iwe bora zaidi ya TANU na AFRO SHIRAZI. Kikawa chama chenye mpango, utaratibu wa kupigiwa mfano katika masuala ikiwemo demokrasia ndani ya chama.
Matukio yaliyojitokeza hivi karibuni kuhusumiana na mchakato wa kutafuta mgombea Urais wa chama cha mapinduzi mnayafahamu.
Nilipata fursa kuyachambua ili kila mtu afahamu tulipifika ndani ya CCM. Nikisema mchakato ndani ya kamati kuu ya halmashauri kuu ya chama ulikuwa na.matatizo ya kimsingi: katiba haukufuatwa kuipa kamati kuu fursa ya kuwasikiliza watia nia mmija mmoja, kuwahoji, kuwachambua na hatimaye kupendekeza majina matano. Haya hayakufanyika kabisa.
Kamati ya maadili ambayo ni kitengo ndani ya ofisi ya katibu mkuu ndiyo iliwachuja wagombea. Hivyo wagombea 38 waliishia mlangoni. Huu ni ukiukwaji.
Mchakato wa kidemokrasia ulianza mwaka 1995 ambapo wagombea 16 walipata fursa ya kidemokrasia ndani ya kamati kuu na majina 6 (wakati huo) Utaratibu huu pia ulirudiwa mwaka 2005 ambapo wagombea walikuwa 11 na wote walipita mbele ya kamati kuu na wakapendekezwa 5. Mwaka huo mzee John Malecela hakuridhishwa na kutokuwemo kwenye majina matano na akaomba kukata rufaa halmashauri kuu. Aliruhusiwa na akasikilizwa japokuwa rufaa yake haikubatilisha maamuzi. Hii.ndiyo demokrasia tofauti na ilivyokuwa mwaka huu ambapo watu fulani walikaa na kuamua.
Katika historia yangu, pale ambapo naona kwamba katiba inachezewa, inavunjwa au inakusudiwa kuvunjwa huwa nasema waziwazi. 1972 nikiwa mkuu wa mkoa wa Singida na mbunge kwa kofia ya ukuu wa mkoa nilipinga wazi ndani ya corcas hatua ya kuilazimisha katiba kukidhi mahitaji ya watu binafsi kwasababu wapo watu kadhaa waliokuwa wabunge wa kuchaguliwa na mawaziri na wakateuliwa kuwa wakuu wa mikoa na hawakutaka kupoteza ubunge kwa mujibu wa katiba. Kitendo kile kilinigharimu marafiki, imani ya serikali iliyotaka niitetee na hata nafasi.
Mimi sikubaliani na uvunjwaji wa taratibu na kwa maana hiyo sikubaliani  na kilichotokea Dodoma kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais. Iikuwa ni kukiuka katiba, kuwadhalilisha watia nia wa CCM ambao chama kiliwaruhusu wazunguke nchi nzima wakitafuta kuungwa mkono.
Waliodhalilishwa wamenyamaza kimya isipokuwa watu kama Profesa Mwandosya ambaye alisema wazi kuwa alidhalilishwa. Nawapongeza sana Alhaj Kimbisa, Dr Emmanuel Nchimbi na Bi. Sofia Simba kwa kusema ukweli japo leo hii wanapata tabu sana.
Sisi tuliojenga chombo cha ukombozi wa wananchi hatutakaa kimya.
Nimalizie sasa kwa kusema kuwa kwa kuwa uongozi wa sasa wa CCM umeamua kukibinafsisha chama na kufanya wayatakayo kwa maslahi ambayo sifahamu ni ya nani nasema sikubaliani nayo kwasababu hii siyo CCM niliyoijenga. Kuanzia leo naachana na chama cha mapinduzi.
Uamuzi wangu utawasumbua baadhi ya watu. Makada, wazee wenzangu hata vijana pia. Lakini ni uamuzi ambao lazima niufanye kwasababu vinginevyo nitajisaliti. Kazi ya kulea chama ni kulea katiba.
Pili, sikusudii kujiunga na chama chochote. Nimekuwa mwanaharakati ndani ya TANU na CCM kwa miaka 61 na inatosha sasa.
La tatu, mimi ni raia huru na nina haki zangu za kisiasa, kijamii. Nitaendelea kuwa na misimamo kuhusiana na nchi yangu. Katika hali ya sasa lazima nitoe msimamo wangu. Yapo makundi mawili: moja linasema kidumu chama tawala-maana yake hakuna mabadiliko. Kundi lingine linasema tunataka mabadiliko.
Kwa jinsi ninavyotazama vijana walio wengi wanataka mabadiliko ukiondoa wale vingozi wa UV-CCM. Akina mama, wakulima, wavuvi,wafanyabiashara, wachimba madini, wanafunzi wa ngazi ya chini hadi ya juu wanataka mabadiliko.
Niliulizwa wakati fulani je, nitamuunga mkono nani kwenye Urais na nikssema ni yule anayeungwa mkono na wengi kama ambavyo Mwalimu Nyerere alituasa kuwa tuwasikilize wananchi wanasema nini. Lazima mgombea awe anakubalika ndani na nje ya CCM.
Kutokana na hali hii mimi nipo upande wa MABADILIKO ambayo kimsingi yamechelewa kuja. Sababu zangu ni hizi:
a. Huko nyuma kwenye TANU, AFRO SHIRAZ na CCM ya awali tulikuwa tunatafuta mabadiliko.
b. Ndani ya CCM tuliasisi mabadiliko ya kisiasa mwaka 1992 kwa kuleta mfumo wa vyama vingi.
Kwa ufupi niseme kuwa wakati wote tumekuwa upande wa mabadikiko isipokuwa CCM ya sasa anbayo leo hii inabadilisha hata msemo wa chama kutoka "kidumu chama cha mapinduzi" na kuwa "kidumu chama tawala". Ukiritimba wa chama kimoja umetosha kama tunataka kwenda mbele.
Kuna msemo kuwa "Absolute power corrupt absolutely". Hii imetokea ndani ya CCM. Baada ya kuwa madarakani kwamiaka mingi hakiwezi kuleta jipya pamoja na ahadi za Magufuli aliyepata nafasi ya kugombea urais baada ya katiba kuvunjwa.
Kuongoza nchi ni sawa na kupanda mlima kunakohitaji pumzi. Chama cha Mapinduzi kimeishiwa 'pumzi' ya kuongoza nchi.
Wakati Mkapa anaachia madaraka uchumi wetu ulikuwa unakua kwa 7% kutoka 4%. Kikwete alipikra madaraka uchumi ukiwa unakuwa kwa 7% na anamaliza baada ya miaka kumi uchumi wetu ukikua kwa karibu ya 7%. Hii ina maana tumerudi nyuma ukilinganisha na rasilimali hasa watu walioongezeka kwa idadi ya milioni 10. Hii ni ajabu.
Mwaka 2005 tulisema maisha bora kwa kila mtanzanaia lakini leo hatuthubutu kwasababu tutagombana na wananchi. Tunahitsji pumzi mpya sasa. Mabadiliko ni lazima. Sitaki chama changu cha zamani (CCM) kibadilike ila kikae pembeni kijitathmini kwasababu kimekwama.
Ulaya, Marekani, China wanasema ukuaji wa uchumi lazima ufikie angalau kwa 10% lakini CCM haiwezi kutufikisha huko ikiwa imeshindwa angalau kwa miaka 10 sasa.
Tunahitaji mabadikiko ya uhakika yatuletee ajira, afya bora, elimu bora n.k. Ndani ya CCM kuna ilani nzuri sana na mimi nimekuwa mwandishi wa ilani za CCM na mikakati ya CCM kwa maendeleo lakini ndani ya chama hakuna muda wa kukaa, kujadili na kutekeleza mikakati.
Wanaotaka kujidanganya kwamba wataleta mabadiliko shauri yao lakini wanaotaka mabadiliko ya hakika lazima wakiweke chama kipya madarakani na CCM kiwe chama cha upinzani.
Akina mama, vijana, wazee msipofanya maamuzi leo shauri yenu. Mtaendelea kutengeneza matabaka ya walio nacho na wasio nacho.
Nihitimishe kwa kusema kuwa tumefika mahala pagumu. Nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa sana lakini kwa utafiti wa mzee kama mini ni kubwa kuliko hivyo watu wasife moyo.
Asanteni kwa kunisikiliza.