Baadhi ya mahujaji kutokea Mecca Saudi Arabia wameanza kurejea Tanzania…(Audio)

.
.
Ni Moja ya Habari zilizogusa Vichwa vingi vya Habari Duniani  September 24 2015 imeripotiwa Taarifa kuhusu watu zaidi ya 700 kufariki kwenye Msikiti Mkuu ambao Waumini wa Dini ya Kiislamu huenda kwa ajili ya Hijjah ambao uko Mecca, Saudi Arabia.
Sasa leo Sept 30, 2015 moja kati ya viongozi wakuu wa dini ya Kiislamu, Hemed Jalala aliitisha waandishi wa habari kuzungumza taarifa hizo…’Kwa kuwa leo ndio tumefika Tanzania tukitokea katika misafara inayotoka kule Hijjah  Saudi Arabia  naamini kuna watu watakuwa wanaaka kufahamu kilichotokea kule Saudi Arabia, ningependa kusema kwamba tunamshukuru tumemaliza ibada hii ya Hijjah katika hali ya usalama sisi kama watanzania lakini jambo la kusikitisha na la kuliza ni kwamba hatukurudi sote ambao tumekwenda kutekeleza ibada hiyo’ – Hemed Jalala
.
.
‘Pamoja na kutekeleza ibada hii kilichotokea mwaka huu  ni jambo la kusikitisha idadi ya watu waliokufa ni wengi mno na tukizungumzia ripoti za mwisho ni idadi ya watu 4000 kwa hiyo tumewakosa watu ambao walikuwa wakipiga mawe saba kwenye nguzo yaani kumpiga sheta huku njia mbili zikiwa zimefungwa na hapo ndipo watu walipoanza kupoteza maisha’ Hemed Jalala
.
.
‘Sisi na nikiwemo kama Imamu wa msikiti wa Kigogo na moja wa viongozi wa Dini kwakweli tunaibebesha serikali ya Saudi Arabia  kwa uzembe uliotendeka na uliofanyika katika tukio hilo, kwanini linabeba kwanza ziko barabara kubwa ambazo hazipungui mita 300 kwanini mahujaji hawakuruhusiwa kupita katika barabara zile, la pili sehemu na hili ni muhimu vilevile sehemu ile iliyokuwa imezungukwa na camera nyingi hivi zile camera zilikuwa haziona tukio hili linaloendelea kwa hiyo huo ni uzembe uliojitokeza katika Ardhi ya Mecca ili limebebwa na serikali na wenyewe wamekubali’ – Hemed Jalala
 Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Sheikh Mkuu wa msikiti wa Kigogo Dar es Salaam