Muhongo: mfanyakazi Tanesco atakaye fanya madudu tutamtupa nje

Serikali imesema haitamvumilia mtumishi yeyote wa shirika la umeme nchini TANESCO au wakandarasi wanaopewa kazi na shirika hilo katika usambazaji wa umeme vijijini atakayewalaghai wananchi na kuwaomba rushwa kama njia ya kumsaidia katika kufanikisha zoezi hilo kwa mwananchi huyo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo katika kijiji cha Kitaramaka wilaya ya Bunda mkoani Mara katika ziara yake ya kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini unaotekelezwa na wakala wa nishati ya umeme vijijini.
Amesema katika kufanikisha zoezi hilo kwa vijiji 1500 katika mikoa 25 Tanzania Bara vitendo vya rushwa haviruhusiwi kwa mtumishi yeyote wa Shirika la Umeme nchini TANESCO au Wakandarasi wanaotekeleza mradi huo.