Waalimu walalamikia kutolipawa mapesa yao



WADAU wa elimu na baadhi ya walimu mkoa wa Njombe wamesema kuwa kama serikali haita timiza matakwa yao watafanya mabadiliko mwaka huu hasa kwa kurekebisha mishahara kwa walio panda madaraja.

Hayo yamebainishwa, Mkoani Njombe, wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Njombe, ambapo kwa jimbo la Njombe kuna mgombea Emmanuel Masonga, wadau hao walisema kuwa watafanya mabadiliko kama serikali itaendelea kuto wajali.

Mmoja wa walimu walio hudhuria katika mkutano huo na kusikia sera ya elimu inayo nadiwa na Chadema, Frances Manga, alisema kuwa serikali kama haita walipa ongezeko la mshahara  kwa walimu waliopanda madaraja mwezi wa mai mwaka huu na kuwa kwa mkoa wa Njombe hasa halmashauri ya mji huo kunawaalimu wanapandisha madaraja wakiwa na  miaka mitano kazini tofauti na sera ya ajira ya taifa.


Alisema kuwa mwisho wa mwezi ulio pita kama katika mishahara yao hakuta onekana ongezeo lolote la mshahara watafanya mabadiliko ili kuitoa serikali ya chama cha Mapinduzi kwa maana kimewakandamiza vyakutosha.

Alisema kuwa walimu wakekuwa hawaonekani kama wanamuhimu kwa taifa hili kwa kuwa maombi yao hayatekelezwi kwa wakati na kusema kuwa kuna mgomo wa chini chini katika mashule hapa nchini.

Mwalimu Manga alisema kuwa wamekuwa wakidai pesa zao kwa mda mrefu na mamlaka zinazo husika kama Halmashauri na TSD wanapigiana mipira na kuw awameahidiwa mwisho wa mwezi Agosti watapatiwa pesa zao na kupewa barua ambazo zinaonyesha wamepandishwa madaraja tangu mwezi Mai mwaka huu.

Mgombea ubunge, Emmanuel Masonga Aidha akiwa jukwaa Mgombea ubunge kwa Chadema jimbo la Njombe kusini Emmanuel Masonga (Pichani) alisema kuwa sera za Chadema ikishiga dola kutakuwa na ufuatiliaji wa hali ya juu masuala ya elimu.

Alisema kuwa sera ya chama chao taifa inasema kuwa kipaumbele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu ni elimu.

Alisema akiingia bungeni atahakikisha kuwa walimu na sekta zingine watu hawalalamiki kwa kupunjwa mishahara amba kwa kuonewa na waajili kwa kuwa watakuw awakiyapokea matatizo yao moja kwa moja na kuyawasilisha serikalini hasa kwa kuwa watakuwa na makao yao kwa wananchi.  

“Mimi nitakapo kuwa mbunge itakapo kuwa elimu bure nitasaidia elimu kuboresha katika sekta ya umma na sio katika sekta binafsi na ubura kuikomboa njombe,” alisema masonga.

Alisema kuwa bila kuwapo kwa elimu hakuna kilimo chenye tija na kuwa elimu itasaidia kuinua kilimo, alisema kuwa kila mwisho wa bajeti ya Tanzania kumekuwa na mswada wa sheria ya fedha lakini Wabunge wamekuwa hawapati uwakilishi wa ukweli kuwatetea na kuleta uwiano wa kikodi wa pembejeo za kilimo ili wakulima kulima.