Fuatilia picha 20 Lowasa alivyoingia Njombe mpaka hotuba,
Wakazi wa Njombe Wkisubiri kumlaki Mgombea wa Uraisi kupitia ukawa, Edward Lowassa, ni Maeneo ya stend kuu ya mabasi.
Hadi wazungu
Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge Emmanuel Masonga wa jimbo la Njombe Kusini kushoto
Umati wa wakazi wa Njombe
Baadhi ya mabango ya wakazi wa Njombe
WAZIRI mkuu wa zamani Fredrick Sumaye amesema kuwa mgombea
urais kupitia Umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) waziri wa zamani Edward
Lowassa hakuwa na kosa wakati wa Lichmond alijitoa kafara kwaajili ya nchi na
ndiop maana hakufukuzwa kazi.
Sumaye ameyasema hayo wakati Akizungumza na wakazi wa mkoa wa
Njombe katika mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia Ukawa Mkoani Njombe
alisema kuwa Lowassa hakuwa na kosa na ndio maana aliamua kujiondoa mwenyewe na
kuwa ndio maana hakufukuzwa.
Alisema kuwa kama Lowasa alikuwa ana kosa angefukuzwa wakati
uleule na angechukuliwa hatia kipidi kile na kuwa alijuondoa kwa kulinda
heshima ya nchi.
“Lowassa alijiondoa kwa lengo la kulinda heshima ya Rais na
ndio maana baada ya kutoka hakuna hatua yoyote iliyo chukuliwa, na hata zile za
Escrow Lowassa hakusema kwa udhaifu huo hawata weza kudhuia rushwa ,” alisema
Sumaye.
Lowassa aliamua kujitoa kama kondoo wa Kafara hakuwa na kosa
na kama wakija CCM wawaulize baada ya hapo walifanya nini na hawata weza
Kudhibiti rushwa kwa kuwa Escrow walishindwa.
Alisema kuwa CCM wanapo sema kuwa alihusika anasingiziwa na
kuwa baada ya Lowassa kutoka walifanya nini na kuwa alipo ondoka walichukua
pesa za Escrow walizipeleka wapi?.
Alisema kuwa Rais Jakaya Kikwete mwenyewe alisema wakati wa
Lowasa kujiudhuru alisema kuwa kijana hakuwa na kosa alijitoa kwaajili ya
kuiokoa nchi.
Alisema mkuwa sababu ya yeye kujitoa CCM ni kuwatoa hofu
wananchi juu ya Ukawa na kuwa sababu nyingine ni kuwapo unyonyaji wa pesa za
wananchi na kuwa akiwa madarakani aliiicha nchi kikiwa katika hali nzuri na
sasa wameachwa katika hali ngumu.
Alisema kuwa yeye tangu amekuwa mbunge na kabla hajawa mbunge
hata alipo kuwa waziri alisema kuwa hakukuwahi kupandishwa bei ya mafuta ya
taa.
Alisema kuwa wananchi hawata pata umeme vijijini cha zaidi
wanapewa adhabu ya kupandishiwa mafuta kwa kuwaogopa matajili wenye vituo vua
mafuta.
Alisema kuwa kodi imapo pandishwa huwa haipandishi katika bei
za mafuta ya taa kwa kuwa wananchi wengi wanatumia mafuta ya taa hapa nchini kwa
kuwa hakuna umeme maeneo ya vijiji.
“Mimi nimekaa kwenye bunge kwa mda mrefu huwa hatupandishi
bei kwenye mafuta ya taa kwa sababu wanatumia watu wanyonge na watu masikini,
eti waziri wa fedha bila aibu anapandisha mafuta kwa kuwaogopa wanaochakachua
mafuta,” aliongeza Sumaye.
Aliongeza kuwa kuhusu nchi kuingiza katika machafuko kama
Libya watakuwa wamesababisa CCM kwa kuwa wananchi watawakataa, na kuwa
Wapinzani wataleta machafuko ni uongo.
“Nataka niwaambieni hivi hapo kwanza walikuwa wanajishitaki
Libya na Misri waliingia katika machafuko kwa sababu wale walio kuwa wnatawala
walikuwa wanang’ang’ania katika madalaka, na walikuwa wanataka kuweka watoto
wao,” aliongeza Sumaye.
Mwisho