“PRESS RELEASE” TAREHE 28.08.2015.
·
MTU MMOJA ANAYEDHANIWA KUWA NI MHALIFU
AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI.
·
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA B AADA
YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUCHANA BENDERA YA CHAMA NA KUBANDUA BANGO LA
MGOMBEA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA DAWA YA KULEVYA [BHANGI].
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ANAYEDHANIWA KUWA NI MHALIFU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ATHUMANI ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI
NA ASKARI POLISI WALIOKUWA DORIA ENEO MLIMA NYOKA NJE KIDOGO NA JIJI LA MBEYA
NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA
MATIBABU.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015
MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO
ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA ITEWE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
UCHUGUZI
UNAFANYIKA KUPATA UKWELI WA SABABU ZILIZOPELEKEA MAUAJI HAYO, KWANI ZIPO
TAARIFA ZINAZODAI KUWA MAREHEMU NA WENZAKE WATATU NI BODABODA NA WALIKUWA
WAKISINDIKIZA LORI LILILOKUWA LIMEBEBA SHABA BILA KUWASILIANA NA ASKARI
WALIOKUWA DORIA ENEO HILO AMBALO UWA NA
MATUKIO YA UHALIFU YA MARA KWA MARA.
MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. ASKARI POLISI WALIOKUWA
KWENYE ENEO LA TUKIO PAMOJA NA WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO WANAHOJIWA KUPATA UKWELI.
UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTEMBEA
KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMBINISYE
MWANDOBO (65) MKAZI WA KISEGESE ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA
KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISSION ITETE KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA
PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA KISEGESE, KATA YA KISEGESE, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI. UPELELEZI
UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA/KANUNI/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMANI JOHN @ MWAKASEGE KWA KOSA LA KUHARIBU
MALI [KUCHANA PICHA] YA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015
MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO
ILOMBA, KATA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA
KUWA, MTUHUMIWA ALIONEKANA AKIWA AMEBEBA MABANGO YA PICHA ZA MGOMBEA WA URAIS
HUKU YAKIWA YAMECHANWA VIPANDE VIPANDE NA NDIPO JITIHADA ZA KUMKAMATA
ZILIFANYIKA NA KUMFIKISHA KATIKA KITUO KIDOGO CHA POLISI ILOMBA.
AIDHA
KATIKA TUKIO JINGINE, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FADI MWASHIMAHA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA
KOSA LA KUHARIBU MALI [KUCHANA BENDERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI].
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO IYUNGA,
KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA
KUWA, MTUHUMIWA NA VIJANA WENGINE WALIITOA BENDERA HIYO ILIYOKUWA JUU YA MTI NA
KISHA KUICHANA KWA MADAI KUWA MTI HUO ULIOKUWA UMEFUNGWA BENDERA HIYO NI MALI
YAO.
WATUHUMIWA
WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO HII KUTOKANA NA MAKOSA HAYO.
TAARIFA
ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NSAJIGWA BROWN (23) MKAZI WA ITUNGE 2. AHOBOKILE RUBEN (21) MKAZI WA ITUNGE
NA 3. AYUBU CHURA (25) MKAZI WA
BONDENI – WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM
25.
WATUHUMIWA
YA WALIKAMATWA USIKU WA KUAMKIA LEO
MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO ENEO LA BONDENI, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA,
WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.