Polisi waanza wiki usalama barabarani Njombe


JESHI la polisi mkoa wa njombe kitengo cha Usalama barabarani kimefungua pazia la wiki ya usalama barabarani Mkoani humo ambayo imeanza jana na kumalizika siku ya Septemba 4 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Njombe kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Kelvin Ndimbo alisema kuwa wiki hiyo imeaza Agosti 27 na kumalizika Septemba 2 mwaka huu huku ndani ya wiki hii kutaendesha mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi juu ya kutumia barabara.

 Wanafunzi watatoa elimu kwa wanafunzi wenzao juu ya kuvuka barabara ndani ya wiku hii ili kujua jinsi ya kutumia barabara hasa sehemu yenye kivuko cha pundamiria, na kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri vibao vya kusimamishia magari na kuvuka.

Amesema kuwa mwisho wa maadhimisho hayo kutakiwa na maonyesho ya vipima mwendo ambavyo maarufu kama tochi za kisasa na kuwa katika wiki hiyo kumenza kutumika kwa tochi hizo.

Alisema kuwa jeshi hilo baada ya kupata tochi mpya kutakuwa na ukamataji magari mpya kwa kuwa na askali walio na tochi mbali na walio vaa sale.


"Askali baada ya kutolwa tochi kutakuwa na askali wanao watakuwa waliovaa kiraia na kukuwa na askali walio vaa sali huku wakipishana kwa mita 300 ili kudhibiti wanaopeana taarifa kuwa kunaaskali mbele ili kuwajenga dereva kulinda sheria za barabarani," alisema Ndimbo na kuongeza

"Kwa kufanya hivyo tunalengo la kujenga sheria za barabarani vichwani mwa madereva ili sheria wakati wote inafuatwa, na askali watakao simamisha Magari waliovaa sale na walio bila sale watafanya kazi ya kuwaambia gali fulani likamateni lina spidi kubwa," aliongeza.

Aidha kwa upande wa madereva wameendelea kulishukuru jeshi hilo kwa kufanya kazi na kuwasaidia kuwakumbusha kupunguza mwendo na kufuatia sheria za usalama Barabarani.

Dereva Zawadi Kilembe alisema kuwa askali hao wanafanya kazi kubwa ya kuwakumbusha wakiwa barabarani na kutoa wito kwa askali hao kufanya doria barabarani kila wakati ili kumaliza kabisa ajali za makusudi.