Matokeo kesho asubuhi ya Uchaguzi wa ndani CCM

UCHAGUZI wa kumpata mbunge atakaye simama kugombea majimbo mbalimbali mkoani Njombe Leo umefanyika huku kukiwa na hali ya utulivi katika vituo mbalimbali vya natawi ya chama cha mapinduzi CCM.

Akizungumza na Mtandao huu mkoani Njombe mmoja wa mawakala wa uchaguzi alisema kuwa uchaguzi huo umeendela vizuri na kuwa wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao ndani ya chama.

Image result for CCM HOSEA MPAGIKEalisema kuwa licha cha wanachama kujitokeza kwa wingi pia wanachama wa vyama pinzani nao wamejitokeza kuanglia uchaguzi unavyo endelea na huku wakiishia kuanga majina na utaratiobu huku wengine walio angalia majina yao waliyaon kwa kuwa walihama chm bila kurejesha kadi za chama hicho.

Aidha Katibu wa CCM mkoa wa njombe, Hosea Mpagike (Pichani anaye zungumza) amethibitisha kuendea vizuri kwa uchaguzi huo na kuwa mpaka kufikia majira ya jioni walikuwa wanaendelea kukusanya matokeo kutoka katika vituo mbalimbali vya uchaguzi kutoka katika majombo mbalimbakli ya mkoa wa Njombe.

Alisema kuwa matokeo ya uchaguzi yatatolewa Leo majira ya sa nne mchana kwa kuwa wanaendelea kukusanya matokeo hayo kutoka katika majimbo sita ya uchaguzi ya mkoa huo huku kila jimbo lina zaidi ya vituo 400 ambavyo ni matawi ya chama hicho


mpagike aliongeza kuwa; Katoka mkoa huu kupata matokeo kwa jioni hii itakuwa ni ngumu mpaka kesho majira ya saa nne tutakupa matokeo yote mpaka sasa naendelea na kzi ya kuyakusanya," alisema Mpagike.