Azam Fc Watwa kombe la Kagame

Mabingwa wa wapya wa Kombe la Kagame timu ya Azam FC wakishangilia na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Azam FC wameibuka mabingwa wa kombe hilo baada ya kuifunga timu ngumu ya Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa fainali kwa mabao 2-0. Azam imemal;iza michuano hiyo huku beki zake na mlinda mlango wao wakiwa hawajaruhusu goli hata moja katika lango lao kwa dakika 90 za mchezo.  

Bao la kwanza la Azam lilifungwa kunako dakika ya 16, kupitia kwa  John Bocco ‘Adebayor’ aliyeitendea haki krosi safi ya Kipre Tchetche.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika ambapo timu iliporudi uwanjanani zilecheza kwa kushambukliana lakini bado nyota ilikuwa kwa watoto wa nyumbani Azam FC ambao katika dakika ya 64, Kipre Tchetche akapachuika bao la pili lililodumu hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi Louis Hakizimana wa Rwanda