Wakulima Njombe kupata nafuu ya mazao yao mabichi

SERIKALI wilayani Njombe imesema kuwa imefanya jitihada zake nyingi za kuhakikisha wananchi wanao jihusisha na kilimo cha matunda na mbogamboga wanapata masoko ya uhakika kwa mazao yao yaliyo sindikwa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi ya kutoa elimu ya kusindika Mboga za majani na matunda ya Kijani Kibichi Tanzania, mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba alisema kuwa amekuwa akitafuta mbinu mbalimbali za kuwainua kiuchumi wakulima wa mbogamboga na matunda mkoa wa Njombe.

Alisema kuwa amekuwa akipambana kila kukicha kuhakikisha wakulima hao wanakuwa na masoko ya uhakika wa mazao yao ya mbogamboga na matunda ambapo wakulima wengi mazao yao yamekuwa yakipotelea shambani.

Alisema kuwa kutokana na wakulima kuto kuwa na elimu juu ya usindikaji wa matunda na elimu ya ujasiliamali wamekuwa wakipita hasara kwa mazao yao kuoza na kuishia kulisha kuku na wanyama wengine.
“Mimi ni mtu wa vijiweni sana na huwa vijiwe vyangu ni soko la wakulima pale na badilishana mawazo na wakulima na wakinamama sokoni pale wakulima wengi mazao yao nimekuwa nikishuhudia yakiodha na wakulima hao wanashinda hata kupunguza bei ili auze apate hata faida kidogo,” alisema Dumba.

Alisema kutokana na wakulima kuto kuwa na elimu ya ujasiliamali wamekuwa wakishinda kushusha bei ili apate angalau faida kidogo anaona bora matunda yakaharibika.

Alisema kuwa kuja kwa taasisi ya Kijani kibichi kuta saidia kuinua uchumi wa wakulima wa mbogamboga na wakimanana ambao wamekuwa wakipigana kutoka kutokana na kilimo.

Hivyo ametoa wito kwa wakulima kujiunga katika vikundi ili kufikiwa kirahisi na watoa elimu ya usindikaji wa mazao yao mbalimbali ya kilimo hasa matunda na mboga za majani ili kuinuka kiuchumi na kuwa watu waondokane na dhana ya serikali kuwapa maisha bora bali serikali itazipa sapoti taasisi zinazoonyesha moyo wa kuwasaidia wakulima na wananchi wake kwa ujumla.

Aidha Dumba alisema kuwa hata wana wa Israel walipo kwa jangwani Mungu aliwapa chakula lakini alitaka wafanyakazi kwa kukusanya chakula na kuwa aliwapa chakula lakini hakuwapelekea hadi ndani na kuwataka wakulima kuacha uvivu wa kujifunza mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato.


Kwa upande wa taasisi hiyo imesema kuwa itajikita hufundisha uzalishaji wa kisasa na usindikaji wa mazao mabichi kama mboga za majani, nyanya na matunda mengine.