ABIRIA wa kwenda maeneo mbalimbali kutoka Mkoani Njombe wameshindwa
kusafiri kutokana na mgomo wa madereva unaoendelea Mkoani hapo huku wakiitupia
lawama serikali kuto wasikiliza madereva hao.
Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti Mkoani hapo
wamesema kuwa kuto kuwapo kwa usafiri kutokan ana mgomo huo ni aibu kwa
serikali kwa kuwa mgomo huo ni tabu kwa wananchi.
Mmoja wa wasafiri kutoka Mkoani Mbeya na kuelekea Mkoani Songea,
John Mapunda alisema kuwa hali hiyo ni kero kubwa kwa wananchi na kuwa serikali
iwasikilize madereva ili gari zianze kufanya kazio yake za usafirishaji.
Alisema kuwa mgomo huu unawaadhili sana watu wenye kipato
cha chini kwa kuwa watu wasiposafiri wanaweza kulala nje kwa kuwa kunawengine
walikuwa wanasafari na wamefikia katikati ya safari na pesa kushindwa kuelekea
popote pale na poesa walizo nazo kidogo.
Aidha Abel Ngolochemba alisema kuwa yeye anatokea Makambako kwenda
Njombe mjini na kutumia usafiri wa Noah na kuwa wametozwa pesa kubwa kutoka
nauli ya kawaida ya shilingi 2500 na kulipa 6000, na kuwa serikali itaadhirika
kutokana na wafanyakazi kufika katika ofisi zao kwa kuchelewa.
Alitoa ushauri kwa serikali kuwasikiliza madereva na kuwa
isipo wasikiliza kuna watu watakufa kutokana na mgomo huu na wengine kukosa
huduma muhimu ambazo ilitakiwa kuzipata kwa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda
nyingine.
Kwa upande wao madereva walisema kwua serikali inatakiwa
kuwaita madereva wamesema kuwa wanaotakiwa kukaa na madereva kwa kuwa kuto
kuwapo kwa madereva ambao ndio wanagona
na kukaa baadhi yao.
Mmoja wa dreva ambaye hakutaka kujajwa jina lake alisema
kuwa mgomo huo upo sahihi lakini serikali kitendo cha kuwalazimisha kusoma mara
kwa mara ni kitu ambacho hakizezekani kwa kuwa elimu haitapunguza ajali na kuwa
ajali hizo njingi zao zinasababishwa na madereva wa maroli.
Alisema kuwa serikali ilitakiwa kujadili baina ya madereva
na wadau wengine na kuwa isikae na maafisa wa polisi pekee ili madereva waseme nini
kinawasumbua na nini kina sababisha ajali.
Alisema kuwa madereva wanaolalamikiwa ni bora wangewaita na
madereva wa maroli kwa pamoja na kuwa ajali zingine zinasababishwa na ubovu wa miundombinu,
na kuwapo kwa baadhi ya Trafiki wa tochi wakijifiucha na kujitokeza barabarani
kwa ghafla.
Alisema kuwa serikali kuhusu kusababisha ajali ni bora
ikaangalia usalama kwaza kuliko mda wa kufika safari zao inatakiwa kuangalia
kuwa wamefika salama na kuwa kuangalia wanafika salama bila kujali mda.
Kwa habari zaidi Piga (For More Call us) +255656049045