SERIKALI Mkoani Njombe imewataka wakazi wa mkoa huo
kuhakikisha wanajitoikeza kwa wingi kupigia kura Katiba Pendekezwa kama walivyo
jiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura itakavyotakiwa kuipigia
kura.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Njombe, Sarah Dumba
wakati wa maadhimisho ya siku ya mfanyakazi ambapo wafanyakazi Mkoani Njombe wameungana
na wafanyakazi kote duniani kuadhimisha siku hiyo.
Dumba amesema kuwa wananchi na wafanyakazi wanaotakiwa kujitokeza
kwa wingi kuipigia Katiba Pendekezwa kura ya ndio itakapo tangazwa siku ya
kuipigia kura.
Kwa upande wao wafanyakazi wamesema kuwa wanaomba mkoa huo
ili kuboresha Maendeleo ya mkoa ni vyema miundombinu mbalimbali ikiwemo ya
barabara, mabweni na hospitali.
Akisoma taarifa ya wafanyakazi kwa mkuu wa wilaya Katibu wa
chama cha walimu wilaya ya Njombe Salama Lupenza alisema kuwa mkoa ili kupata Maendeleo
unahitajika kuwa na wasomi na kuwa mkoa huo unawajibu wa kuhakikisha unajenga
mabweni kwa shule zake ili kuendeleza kushika nafasi za juu kielimu kama
ulivyofanya mwaka huu.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika halmashauri ya Njombe kimkoa
na kuhudhuliwa na mamia ya wafanyakazi kutoka wilaya mbalimbali wa mkoa huo
wafanyakazi wameitaka serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa
wafanyakazi ili kuweza kuyamudu maisha.