KUTO kuwapo kwa makazi imara katika kata mbalimbali hapa
nchini kumedaiwa kukwamisha watumishi kufika kufanyakazi katika kata za
pembezoni wakikimbilia mjini kwenye makazi imara ya kuisha.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Makowo halmashauri ya Mji wa Njombe Ojen Mdete wakati Akizungumza katika baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo na kuwa kata yake watumishi katika kituo cha afya hufika na kuodoka kutokana na makazi ya hadhi ya kukaa watumishi hao kuto kuwapo.
Amesema kuwa suala
hilo limesababisha kuto kuwapo kwa huduma katika kata yake kutokana na
watumishi katika kituo cha afya kuto kuwapo.
Mdete amesema kuwa watumishi wamekuwa wakifika na kukaa siku
chache na hatimaye kuondoka na kusikia wamepangiwa kata mahara pengine na
kuwatupia rawama maafisa utumishi kwa kuwahamisha watumishi katika kata yake.
Ameongeza kuwa watumishi wanapo omba uhamisho kuhakikishwe
kuwa wanaona kuwa amapo toka kuna mtu anaye mbadala pale kabla ya kuondolewa
mtumishi huyo ili kutoacha vituo vya kazi bila watumishi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la Madiwani halmashauri
ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga amesema kuwa wananchi wanawajibu wa kushirikiana
na Madiwani wao kuhakikisha miundombinu ya kuishi watumishi inaboresha ili
watumishi wanapoingia katika vituo vyao vya kazi hawatamani kuhama.
Amesema kuwa watumishi isionekane wanakataa mazingira waliyo
pangiwa kazi bali na mazingira Yao ya kufanyia kazi yatazamwe yakoje kwani kuna
mazingira ambayo watumishi wakipelekwa hayafai kuishi hata afisa utumishi
akipelekwa pale hawezi kuishi mazingira ni duni kupita kawaida.