SEKTA ya viwanda hapa nchini ni sekta ambayo ina
muhimu katika Maendeleo kutokana na ajira zinazo tokana na sekta hiyo na mapato
yanayo tokana mapato ya viwanda.
Sasa setikali inatakiwa kujua kuna viwanda vingapi
na mapato yake, ukuaji wake na kujua uendeshaji wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Njombe Meneja
msaidizi wa ofisi ya takwimu ya taifa mkoa wa Njombe na Iringa Respicius Gasper amesema kuwa serikali
inatarajia kufanya utafiti katika viwanda hapa nchini.
Ameongeza kuwa takwimu hizo zinalenga kuboresha sera
ya viwanda hapa nchini na kujua viwanda vingapi vipo hapa nchini na zoezi hilo
limefanikiwa kwa asilimia kadhaa na kuwa kunachangamoto wanakabiliana nazo kama
anavyo eleza.
Amesema kuwa takwimu zinazo kusanywa hazihusishwi na
mamlaka yoyote ile na kuwa zitakuwa ni kwaajili ya ofisi hiyo huku akiwaomba
wamiliki na wahusika wa zoezi hilo kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa
watakwimu.