JUMUIYA ya wafanyabiashara Mkoani Njombe inatarajia
kuambatana na wafanyabiashara wote Mkoani humo kuelekea mjini Dodoma kwenda
kusikiliza kesi ya kiongozi wa jumuiya hiyo kitaifa Jonson Minja.
Inadaiwa kuwa wafanyabiashara Mkoani humo watafunga
maduka na kwenda mjini Dodoma kusikiliza hiyo ambayo itaendeshwa kwa siku tatu
mfurulizo ambapo inatarajia kuanza Juni 8 hadi 11.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa
Njombe, Sifaeli Msigala hivi karibuni baada ya baada ya kumaliza kesi ambayo
ilikuwa inamkabili Mfanyabiashara mwenzao Mexsons Sanga.
Alisema kuwa ataungana na wafanyabiashara wote
nchini kuelekea Dodoma huku maduka yakiwa yamefungwa kwa siku tatu mfurulizo.
Wafanyabiashara wameafikiana kufunga maduka kwa siku
hizo tatu huku wakikemea wasalili ambao wanafungua maduka wakati wanakwenda
mahakamani.
“Wale watakao kuwa wakikweba kodi na huku wapo
katika jumuiya hatuta kubaliana nao kwa kuwa jumu iya hii sio kwaajili ya
kukumbia kodi kazi yake ni kusimamia kodi zote hapa nchini,” alisema
Alisema kuwa kuwapo kwa jumuiya hiyo ni kuhakikisha
kuwa kodi inaliopwa na wafanyabiashara wanafuata kanuni za biashara ili kuto
ikwaza serikali na kuhakikisha nchi inaendelea na kuwa watapambana na wenzao
watakao kwepa kodi.
Aidha Mexsons alisema kuwa tangu awali mkoa wa
Njombe ulijulikana kama shamba la bibi kutokana na upole wa wakazi wa mkoa huo
kitu ambacho hakikuwa maana ya wakazi hao.
“Wakazi wa Njombe zamani TRA walijiwekea kuwa ni
shamba la Bibi ambapo walikuwa wakija na kujichukulia pesa na kwenda kufanya
maedeleo huko ndomana utaona wafanyabiashara wengi walikuwa wanainuka na
kushika, lakini sasa tuamke tuache kutoa rushwa,” alisema Mexson
Aliongeza kuwa wakazi hao pia walikuwa wakiogopa
mamlaka ya mapato tanza nia TRA na wengine kuogoma kufanya Maendeleo na baada
ya kesi yake majengo ya ghorofa kuanza kujengwa.
“Mkoa huu watu walikuwa na fedha zao nyingi tu
walikuwa wanaogopa kusimamisha ghorofa unaona sasa gorofa zinajengwa baada tu
ya mimi kuamka na wao TRA sasa wanaogopa kuja watu wanajenga sasa,” alisema
Mexsons