MBUNGE wa jimbo la Ludewa
Mkoani Njombe Deo Filikunjombe katika mpango wake wa kuwalipia ada wanafunzi 25
wa sekondari kwa kila kata jimboni kwake na kuwafanya wananchi wa jimbo hilo
kuukubari na kumuomba kuendelea na utaratibu huo ambao umeweza kuwanufaisha
wanafunzi walio wengi wanaotoka katika mazingira magumu.
Hayo yamebainishwa na
baadhi ya wakazi wa kata za jimbo ni kwake ambapo Mmoja wa wananchi wa kata ya
Mavanga John Haule alisema kuwa awali kabla ya Filikunjombe kuingia madarakani
watoto yatima walitegemea sana mashirika yasio ya kiserikali kuwasaidia katika
kulipia gharama za masomo.
Hivyo watoto hao kukwama
kuendeleza na elimu kutokana na mashirika hayo kuto kuwa na mda mrefu wa
misaada yao.
Haule alisema kuwa tokea
alipoingia madarakani Filikunjombe ndani ya miaka mitano ameweza kuwalipia ada
wanafunzi ambao wamefanikisha kuhitimu masomo yao kwa ngazi ya kidato cha nne
na waliofanikiwa kufaulu ameendelea kuwapa msaada kwa kuwalipia ada katika
ngazi ya kidato cha tano.
Alisema wilaya ya Ludewa
yenye kata 26 wameweza kusaidiwa zaidi ya wanafunzi 700 ambao mpaka sasa kuna
wengine wameweza kujiunga na fani mbalimbali za ufundi baada ya kuhitimu kidato
cha nne lakini kubwa zaidi wamekuwa wakikumbuka mchango wa mbunge wao katika
maisha yao kwa kumpokea kwa shangwe na kumpa zawadi mbalimbali pale anapotembelea
vijijini hali ambayo imemtia moyo mbunge huyo na kuona mpango wake umefanikiwa
kwa kiasi kikubwa.
“Mpango wa Filikunjombe
umefanikiwa kwa asilimia miamoja kwani tumeanza kuyaona matunda yake lakini
wakati anaanza na mpango huu wa kuwalipia ada wanafunzi wa mazingira magumu kwa
kuwaagiza viongozi wa kata na vijiji kupendekeza majina ya watoto tuliona kama
ni siasa leo hii kila mmoja wetu ameona faida yake hivyo tunamuomba aendeleze
mpango huu kwani ni ikombozi wakielimu katika wilaya yetu”, alisema Haule.
Katibu wa Itikadi na
uenezi wa chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Njombe Onoratus Mgaya katika ziara
ya mbunge huyo kata za Mavanga, Ngelenge, Mawengi na Lupanga alisema licha ya
kuwalipia ada za shule watoto wa mazingira magumu pia Filikunjombe amekuwa ni
mfano wa kuigwa nchini kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi katika jimbo
lake kwa muda muafaka hali ambayo imekuwa ikikipa sifa chama na kuwafanya
wananchi kuendelea kukipa nafasi ya kuendelea kushika dora miaka mingi ijayo.
Akizungumza katika
mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya
Mavanga Mgaya alisema kuwa CCM sio chama kibaya kamabaadhi ya wanasiasa wengine
wanavyosema ila kunawatu wako ndani ya ccm ni wabaya na mkakati wa chama ni
kuwaondoa watu hao haraka iwezekanavyo ili kusikiliza vilio vya wananchi kwani
wananchi wanahitaji maendeleo na si porojo.
Aidha akizungumza na
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mavanga Filikunjombe alisema kuwa mpango
wake wa kuwalipia ada wanafunzi ulikuwa wa majaribio lakini kabla haja fanya
utafiti wa majaribio yake ameshayaona mafanikio makubwa ambayo hakuyatarajia
kutokana na kila kijiji anachopita amekuwa akipata mapokezi makubwa na zawadi
kwa baadhi ya wanafunzi aliyowasaidia.
Filikunjombe alisema
licha ya kutoa msaada huo wa wanafunzi wenye mazingira magumu pia amekuwa
akiwasisitiza wazazi kuwapeleka watoto shule ili mwisho wasiku waje kuwa
viongozi wa wilaya hiyo kwani yeye si mbunge wa milele katika jimbo la Ludewa.