YAMOTO BAND WATINGA RADIO KASIBANTE 88.5 FM BUKOBA TAYARI KWA SHOW YAO USIKU HUU NDANI YA LINA'S CLUB


Na Faustine Ruta, Bukoba
Kundi zima la Yamoto Band punde walitinga Katika Kituo cha Radio Kasibante 88.5 Bukoba kuongea moja kwa moja na Wakaazi wa Bukoba juu ya Shoo ya yao inayotarajiwa kufanyika Usiku huu katika Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night Bukoba. Bendi inayokuja kasi hapa Nchini inayoundwa na Vijana Machachari kama Aslay, Becka, Bella na Maromboso wameteta na Wanabukoba kwamba waje kwa wingi katika Ukumbi huo wa Lina's wajionee walichokuja nacho kipya katika Pasaka hii ya pili maana kwa sasa watawasha Moto wa Uhakika na Watatoa Burudani Live jukwaani na wamekuja wamejipanga wakiwa na Vijana wengine ambao ni Maalum kwa Kuliteka Jukwaa kwa mapigo ya Live"
Mtandao huu wa jamii murua kwa habari tamu za Michezo na Burudani pia umeweza kuzinyaka za haraka haraka kwamba baada ya Shoo ya leo katika Ukumbi wa Lina's Kesho Jumatatu watatoa Burudani pia huko Biharamulo kwa kiingilio cha 10,000/ siku ambayo ni Karume Day" ya jumanne tarehe 07/04/2015. Kiingilio cha Shoo ya leo ya Lina's kwa kawaida ni Tsh 10,000/ na VIP ni Tsh.15,000/-
Wasanii wa Kikundi cha Yamoto Band wakiwa Katika Studio za Radio Kasibante 88.5 FM kuteta na Mashabiki wao na kuwajuza Kile walichokuja nacho kwa mara nyingine na kwa mwaka huu mpya wa 2015.
Wasanii wa Yamoto Band wakiwa wanaimba moja ya Wimbo wao mpya wa "Nitakupwelepweta" katika Studio za Kasibante 88.5 FM
Jonathan Mwanga maarufu kwa Jina la Jerry ambae ndie muhusika Mkuu wa Show itakayofanyika baadae usiku huu aliyewaleta kwa mara ya pili Yamoto Band hapa Bukoba nae alikuwa Sambamba na Wasanii hao wanaokuja kwa kasi hapa Nchini.
Usiku huu Moto wa Yamoto band Kuwaka!!
Pamoja sana..!
Mtangazaji wa Radio Kasibante FM 88.5 Jerome akiwa live kwenye kipindi na Vijana wa Yamoto Band
Slay akiongea moja kwa moja na Mashabiki wake kupitia Radio Kasibante 88.5 FM Bukoba leo hii jioni