MKUU wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amewapa hamasa vijana wanao fanya kazi za bodaboda kwa kuwapa zawadi baadhi yao Pasaka hii licha ya kazi hiyo kuonekana kutoungwa mkono na baadhi ya wanajamii na kusema kuwa wanaoifanya kazi hiyo ni wahuni.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi hizo mwanzoni mwa wiki hii mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Nchimbi amesema kuwa kazi ya bodaboda ni baraka na si ya kihuni kama wanavyosema baadhi ya wanajamii kwa kuwa kunawatu wanasomesha ndugu zao kutokana na kazi hiyo.
Amesema kuwa waendesha bodaboda walio wengi licha ya kutofika elimu ya sekondari lakini wamekuwa kipaumbele kulipia michango mbalimbali ya sekondari za kata na kulipia ada za ndugu zao kupitia kazi hiyo.
Aidha kwa upande wao madereva wa bodaboda mbali na kushukuru zawadi hizo za kuku na mchele kwa baadhi yao wamesema kuwa ajali nyingi zinazo tokea zinasababishwa na baadhi ya watumiaji wa barabara wasio makini na kwa baadhi yao kuwapa waendeshaji wa muda maarufu daywaka.
Emelamu Msigwa ni mmoja wa madereva ambaye amesema kuwa ajali nyingi zinazo tokea zinasababishwa na wale wanaopewa kwa muda pikipiki wakati dereva anapo kuwa amechoka.