Ukosefu wa uelewa wa sheria wawakosesha imani watanzania

Watanzania wengi bado wanakosa imani juu ya hukumu zinazotolewa kwao na vyombo vya sheria kutokana na uelewa mdogo wa sheria pamoja na kukosa wasaidizi wa kisheria ambao wangewasaidia.
Hayo yamebainishwa na wasaidizi wa kisheria (Paralegal) kutoka halmashauri mbalimbali nchini ambao wanakutana jijini Dar es salaam kufanya tathimini ya miaka miwili toka kuanza kwa mradi wa kuwaandaa wasaidizi wa kisheria, unaotekelezwa na mfuko maalumu wa kusaidia mashirika yanayotoa huduma ya kisheria kwa wananchi, chini ya ufadhili wa Serikali za Tanzania na Denmark.
Wasaidizi hao wa kisheria ambao wapo kwenye halmashauri zote za Tanzania Bara na Zanzibar wamesema, mashauri mengi wanayokutana nayo kutegemea na eneo husika ni pamoja na masuala ya ardhi hasa kwa wanawake, matatizo ya ndoa na matunzo kwa watoto pamoja na changamoto wanazokumbana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwemo serikali kutowatambua lakini pia umbali kutoka walipo hadi kwa wananchi wenye mahitaji.

Related Posts