Kilichotokea Simba baada ya ajali na matokeo ya mechi za VPL

 

Baada ya klabu ya Simba kupatwa na msiba wa kupoteza mashabiki 5 katika ajali iliyotokea jana – mechi yao dhidi ya Kagera Sugar iliyokuwa ichezwe leo imeahirishwa na sasa itachezwa Jumatatu.
Taarifa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania zimeeleza mechi hiyo iliyokuwa ipigwe leo kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imeahirishwa kutokana na ajali ya mashabiki wa Simba Ukawa.
Mashabiki watano na watu wengine wawili walipoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea jana katika eneo la Dakawa mkoani Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea wakati mashabiki hao wakiwa wanakwenda kuiona mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.
Katika hatua nyingine Ligi kuu ya Vodacom imeendelea leo hii kwa Ndanda FC ambao waliikaribisha Mbeya City Mtwara na kutoka sare ya  1 – 1 Mbeya City, Coastal Union wamefungwa nyumbani 0 – 1 na Prisons, huku Ruvu Shooting  wakiitandika 1 – 0 JKT Ruvu