Chama cha ushirika Njombe Njorecu Chaonywa viongozi wanasiasa

MRAJISI wa vyama vya ushirika Tanzania Dkt, Audax Lutabazibwa amewataka viongozi wa vyama vikuu ya ushirika hapa nchini kutekeleza mabadiliko ya sheria mpya ya vyama hivyo.

Sheria mpya ya vyama vikuu ya ushirika ina weka mbali siasa na viongozi wake ili kufanya utendaji wake kuwa madhubuni na kuwa seria hiyo hairuhusu kiongozi kujihusisha na siasa.

Akizungumza kwa niaba ya mrajisi mkuu  huyo katika mkutano mkuu wa vyama vya ushirika mkoa wa Njombe (Njurecu) Mrajisi msaidizi wa chama kuku cha ushirika mkia wa Iringa, John Kiteve alisema kuwa kuna sheria imeunda ili kudhibiti viongozi wa vyama hivyo kujihusisha na siasa ili kuepusha mkanganyiko ndani ya vyama hivyo katika utendaji.

Kiteve alisema kuwa hali hiyo imelenga kutenganisha miingiliano ya kiutendaji na siasa wakati wa kutekeleza majukumu ya chama na kuwa wanachama wa kawaida hawazuiwi kuwa wanasiasa.

Hiyo aliwataka wanachama wanao taka kugombea katika nafasi yoyote ile katika vyama hiyo kuhakikisha kuw hawajihusisi na siasa ili kwenda sawa na sheria hiyo na kuwa kaka kiongozi akigombea na kubainika anajihusisha na siasa atapokwa nafasi yake.


Akisoma taarifa ya ushirika huo mwenyekiti wa chama hicho ambaye alikuwa kiongozi na kuchaguliwa tena kwa awamu nyingine, Clemence Malekela alisema kuwa licha ya uchanga wa chama hicho kimefanikiwa kupiga hatua kubwa katika kukuza kwa kuwafikia wanachama na kuwapa elimu juu ya umuhimu chama hicho.
Mwenyekiti aliyekuwa akitetea kiti na kushinda Clemence Malecela


Malekela alisema pamoja na mafanikio ya kupata soko   la mahindi kwaajili ya wakulima lakini serikali imewakwamisha  wakulima   hao   kwa   kuchelewa   kuwa lipa   wa kilima   fedha   zao   za   mazao.
 

Hata hivyo chama hicho kimefanya uchaguzi ili kuwapata viongozi wapya kwa sasa ambao watafanyakazi ya kuendele zaushirika huo.

Katika uchanguzi huo viongozi walichaguliwa na mwenyekiti wao wa msimu wa kwanza na wajumbe watatu kuongezwa katika bodi ya uongozi kutoka sita hadi tisa bodi hiyo ya uongozi wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Njombe.