Mapya yaibuka Ndege ya Germanywings iliyoanguka mlimani



GermanTaarifa nyingine kuhusu ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika Milima ya Alps Ufaransa siku ya Jumanne March 24 zinasema kulingana na uchunguzi uliofanywa kwenye kisanduku cha kunasa sauti katika ndege hiyo inaonesha rubani mmoja aliyekuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege amehusika kusababisha ajali hiyo.
BN-HO782_0325fr_H_20150325082229Uchunguzi wao unaonesha rubani huyo alimfungia rubani mwenzake nje ya chumba cha marubani na kuipeleka kwa kasi ndege hiyo eneo lenye milima hiyo na kuigongesha huku abiria wakisikika wakipiga kelele kabla ya ndege hiyo kuanguka.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 ilikuwa ikitoka Barcelona kuelekea Düsseldorf Ujerumani, iligonga Mlima na kuwaua abiria wote 144, pamoja na wafanyakazi sita wa ndege hiyo, maafisa usalama wa Ufaransa wanasema rubani Andreas alikuwa hai mpaka hatua ya mwisho ndege hiyo ikipata ajali.
Bado hawana uhakika kusema chanzo hasa cha ajali japo Serikali ya nchi hiyo imekataa kuthibitisha kwamba tuio hilo lina uhusiano na masuala ya kigaidi.
Kinachoangaliwa kwa sasa ni jinsi ya kuweka utaratibu mpya wa kuwepo Sheria itakayowafanya Marubani wote wawili kuwepo ndani ya chumba cha marubani wakati wote ndege ikiwa safarini.