Lwenge: Mda wa kampeni bado!!!!!!!!!


MBUNGE la Njombe Magharibi Gerson Lwenge ametoa onyo kwa wanasiasa ambao wameanza kupiga kampeni wakati yeye bado hajamaliza mda wake wa ubunge hasa kampeni za usiku na kununuliwa kwa pombe wa wananchi wake.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara zake za Vijiji kwa vijiji katika kata za jimboni humo, Lwenge alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu wa aina hiyo.

“Wananchi muwe makini na watu wanao kuja na kuwapa pombe katika kampeni zao za usiku kwa kuwa mda wa kampeni bado haujafika na mtafakali ni kwan ini wanapiga kampeni za usiku,” alisema Lwenge.

Kwanza wananchi mnatakiwa kutafakari ju ya watu wanao kuja katika maeneo yenu usuku na kuwanunulia pombe na kuanza kuwaambia mmchague kwani watu hao wanawanunulia pombe lakini pombe hamuwezi kwenda nazo katika nyumba zenu.

Alisema kuwa mtu akiwafuata na kuwaambia wamchague wamuulize kuwa amewafanyia nini kwa kuwa wakati wa kuambiwa watafanyiwa mda huo ulipita.

“Wananchi wakati wa kuambiwa mtafanyiwa wakati huo ulipita miaka ya nyuma, katika kipindi change kuna vijiji vitapatiwa umeme zaidi ya 40 lakini miaka ya hapo nyuma wabunge wawili walipita na vijiji tisa vilipata umeme, na shule mbili zilipatiwa umeme lakini kwa sasa shule zote za kata zitapatiwa umeme,” aliongeza Lwenge.

Alisema kuwa katika kipindi chake vijiji vingi vimepata umeme tofauti na miaka ya utawala wa wabumbe wa kabla yake na kuwa katika utawala huu vijiji vichache vitachelewa kupata umeme na kupatiwa katika awamu ya tatu.

Alisema kuwa pia katika kipindi hiki amefanikiwa kuwapelekea barabara wananchi kjwa kiwango cha changalawe na lami kwa baadhi ya maeneo katika jimbo hilo na kuwa wananchi kwa mda huu wanaweza kuunganishwa kwa mtandao wa barabara.