UMOJA wa wafanyabiashara  wa Mbao mkoa wa Njombe Uwambanjo  umehamasisha wafanyabira hiyo kuandamana huku wakizulu eneo la barabara inayounganisha eneo la soko la mbao na barabara kuu ya Njombe Songea wakishinikiza serikali kuikarabati Barabara inayo ingia sokoni hapo kutokana na uharibifu unaotokana na mvua sinazo endelea kunyesha.

Wafanyabiashara hao waliamua kupiga kambi katika eneo la barabara hiyo mbovu kwa muda, kwa kile ambacho wamesema wanasubiri kuona serikali inachukua hatua za kuikarabati katika maeneo korofi Kabla ya kuandamana mpaka ofisi ya mkurugenzi endapo utekelezaji usingi kamilika.

Wakizungumza na NIPASHE Mkoani hapa mwishini mwa wiki iliyopita, baadhi ya wanyabiashara hao walisema kuwa licha ya kupeleka malalamiko yao katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashairi ya mji wa Njombe lakini hakuna hatua ambazo zinachukuliwa jambo ambalo linapelekea magari yanayofika kupeleka na kununua mbao kukwama na kuwasababishia hasara.

Walisema kuwa wamekuwa wakiingia hasara ya kushusha na kupakia upya mbao pindi gari zinapo kwama katika barabara hiyo ili gari hiyo kupata urahisi wa kujpita katika tope.

Mfanyabiashara Ausebio Mwajombe alisema kuwa awali walikuwa wakipitisha magari hayo katika barabara ya Magereza kutoka marabara kuu mpaka soko la mbao Kambarage ambapo barabara hiyo ilifungwa na mkandarasi ambaye alikuwa anaifanyia matengenezo kwa kiwango cha rami.

Alisema kuwa baada ya kuhamishiwa katika barabara ya Shipo mpaka Kambarage kutoka barabara kuu kabla ya msimu wa mvua ilikuwa ikipitika na baada ya kuanza mvua barabara hiyo imekuwa ni kikwazo cha biashara zao.

Mwajombe alisema kuwa walitoa taarifa kwa halmashauri ya Mji Njombe na kuahidiwa kurekebishiwa barabara hiyo licha ya kuchukua mda mrefu bila kuirekebisha.

Alisema kuwa kufuatia uharibifu uliotokea katika barabara hiyo gari zimesimama kuchukua mbao katika soko lao kwa muda wa wiki mbli kwa kuhofia kukwama katika barabara hiyo.
  

Aidha wafanyabiashara baadhi yao wametishia kutoendelea kulipa ushuru endapo serikali haitafanya ukarabati wa barabara hiyo huku wakilalamikia ukubwa wa kodi wanayolipa kwa madai kuwa kila gari linalofika kununua mbao linalipia ushuru wa shilingi laki tatu kama anavyeleza Prudensiana Fute.

"Kama hali itaendelea  hivi hatuta lipa husuru haiwezekani tukawa tuna lipa ushuru mkubwa hivyo lakini huduma zinahuwa hovyo sisi ni ng'ombe wa serikali sasa kama watakuwa wanakamua bila marisho hatutatoa maziwa," alisema Fute


Akizungumzia kadhia hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Njombe Edwin Mwanzinga alisema kuwa uharibifu wa barabara hiyo unatokana na ujenzi wa barabara unaoendelea kuelekea mtaa wa kambarage pamoja na kukiri kuwa jitihada za kuitengeza barabara hiyo mbovu unaendelea

Hata hivyo Mwanzinga alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi na viongozi katika halmashauri yake kuacha tabia ya kupitisha magari makubwa kwenye barabara ambazo hazina uwezo kubeba mizigo mikubwa kwani kwa kufanya hivyo wanaathiri miundo mbinu na kuitia hasara halmashauri na serikali.

Mpaka NIPASHE inaondoka katika eneo la tukio umwahaji wa mawe katika maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na usubufu ulikuwa unaendelea ambao ulikuwa unaendesha na mkandarasi wa halmashauri ambaye hakuwa tayari kuzungumza.