Polisi wadaiwa kuvamia kambi ya wakulima wa chai

JESHI la polisi mkoani Njombe limelalamikiwa kufanya uvamizi katika kambi wafanyakazi wa kiwanda cha chai cha Kibena cha mkoani humo na kuwachalaza viboko wafanyakazi walio kuwa wamelala na pamoja na familia zao na kufanya unyanganyi wa simu huku wengine wakiwakuta wakiwa uchi.

Wakizungumza na Elimtaa kwa nyakati tofauti wafanyakazi wa kiwanda hicho wamesema kuwa jeshi la Polisi lilivamia katika kambi zao ambapo wanaishi na familia zao na kuvunja milango huku wakitoa amri za kuwataka watoke nje na kuwachalaza viboko na kuwapa adhabu mbalimbali za kuruka vichura bila kujali ni mfanyakazia ama ni mwanafamilia wa mfanyakazi.

Mmoja wa wahanga wa kadhia hiyo Vumilia Ngewe alisema kuwa yeye alitoka kazini saa 12:00 asubuhi ambapo aliingia kazini hapo usiku wa kuamkia asubuhi ya juzi.

Akisimulia mkasa huo kwa shida kutokana na kipigo alicho kipata na kunyanganywa simu yake alisema; “Asikari walikuja usiku majira ya saa 9 wakati tupo kazini walitukuta sisi tunataka kutoka kwa sababu boila ilikuwa imezima kitu kilicho tulazimu kuzima mitambo kiwandani lakini walipo fika ofisini walituamuru tuwashe mashine na tuendelee na kazi huku wengine walioko nje ambao walikuja kwajili ya kutupokea wengine wakipewa adhabu na wengune wakiwekwa pembeni,” alisema Ngewe

Alisema kuwa Polisi walipo fika katika kiwanda hiki walitoa adhabu kwa baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwepo kiwandani hapo bila ya kuuliza kunanini huku maswaliyao yakiwa ni kujua kwa kila mtu ratiba yake ya kuja kazini.

Ngewe alisema kuwa yeye na wenzake ulipo fika mda wa kutoka kazini walitoka na wakati wakutoka polisi waiingia kiwandani humo na kumwambia kiongizo wao katika zamu yao na kumwambia umefunga vizuri ofisi kisha wakaona walio kuwa wanatakiwa kuingia zamu majira ya saa 12:00 asubuhi wakiwa wanalia na kusema wenzao wanaadhibiwa kwa kupigwa na kugalagazwa katika tope.

Alisema walipo fika katika geti la kiwanda hicho walikuta wenzao wakipigwa huku wengine wakiwa hawatambuliki nyuso zao kwa kuwa walikuwa wametapakaa tope usoni na kupigwa ambapo walikuwa na majeraha mbalimbali na wao kuamurishwa kwenda katika kambi zao wanazo ishi.

Alisema kuwa chanzo cha polisi kufika katika kiwanda hicho ni mabosi wao ambao walitakiwa kukaa nao kikao majira ya saa 3:00 asubuhi, na kubadirisha tangazo la kikao hicho na kuwa saa 9:00 kitakaliwa kikao hicho kinyume na makubaliana yao katika kikao chao cha tarehe 3 mwezi huu ambapo kamanda wa polisi aliwataka siku hiyo kuto fanyakazi na kuwa itakuw ani siku ya kikao.

“Kikao chetu kilitakiwa kukaliwa leo (juzi) saa 3 asubuhiu na ndio maana wenzetu wengine wamewahi kuja hapa kiwandani ili kuwazuia wengine ambao walitakiwa kuingia asubuhi kuwa kuwa kamanda wa polisi alivyo kuja Januari tatu katika mkutano wetu na kutuambia siku ya leo hakutakuwa na kazi yoyoto na kazi zitaendelea baada ya kikao, ratiba ya mkutano kuwa saa 9 imebadilishwa wakati wengine walikuwa hawafahamu” alisema Ngewe.

Aidha mama huyo alisema kuwa baada ya kwenda nyumbani katika hizo kambi zao alikumbwa na kizazaa baada ya kusikia king’ora cha gari la polisi kikiingia katika kambi zao na kuanza kuwatoa ndani kwa amri kuwa watoeni waume zenu na kuingia ndani kwa kuvunja milango.

Alisema kuwa yeye kwakua alikuwa ndiyo anatoka kazini aliamuliwa kufungua mlango na kuwaambia kuwa  alikuwa anatoka kuoga alisema polisi walivunja mlango na kumkuta akiwa uchi na kumwambia awaonyeshe mmewe na kuanza kutafuta kama kuna mtu mwingine katika chumba hicho bila mafanikio huku mama huyo akiwa uchi na kisha kuchukua simu yake aliyo kuwa anaitumia kama taa wakati akivaa.

Alisema kuwa polisi walifanya hivyo katika kambi nzima na kuwachalaza viboko wakazi wa kambi hizo bila kujali kuna watoto ama lah na baada ya kuuliza simu yake polisi walikana kuichukua simu hiyo na mkuu wa kikosi kilicho kuwa kikitekeleza zoezi hilo alisema kuwa askali wake sio wezi licha ya mama hiyo baada ya masaa kadhaa kupita kupigiwa simu na kupitia simu yake kwa mdogo wake na kuambia wa unajua unaongia na nanani kisha simu hiyo kuzimwa.

Naye mmoja wa waathilika wa tukio hilo ambaye ni mke wa mfanyakazi kiwandani hapo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa alisikia mabomu yakipigwa kiwandani wakati yeye akiwa kambini kwake na kuwa aliamua kumuuliza mumewe kilicho tokea kazini kwa kuwa alikuwa kambini.

Alisema mumewe alimwambia kuwa hali sio shwari kazini na kuwa alikuwa na ratiba ya kupeleka chai kiwandani hao aliambiwa asiende na baada ya muda fupi alisikia mabomu mengine yakipigwa na kuwa baada ya hapo alisikia king’ora kikilia kuelekea katika kambi yao na kisha kusikia sauti zikiwataka kutoka nje huku nyumba za majilani zake zikuvunjwa milango na kusikiks sauti za vilio.

Alisema kuwa yeye katika nyumba yake alikuwa ametembelewa na nduguzake alivunjiwa mlango na kuanza kuchapwa viboko na askali hao huku wakiondoka na wanaume wote walio kuwa katika kambi hizo na kuwa wakati wakiondoka walikuwa wakiuliza majina ya wale wanaume na kuwatenga huku wakilinganisha na kmajina walikunayonayo.

Mmoja wa wafanyakazi ambaye alikutwa amelala kambini kwake kutokana na homa liliyo kuwa inamsumbua alisema  kuwa aliadhibiwa na askari hao kwa kuchapwa viboko na kuamuliwa yeye na wenzake kutembelea tumbo.

Kwa upande wa chama cha wafanyakazi sekt ya mashambani (Tpau) kanda ya Iringa inayo shughulikia na mkoa wa Njombe, Katibu wake, Deus Magesa alisema kuwa chama hicho kinalaani kitendo kilicho fanyw ana jeshi la polisi kwa kuwanyanyasa wafanyakazi hao kwa kuwa nguvu waliyo itumia haikupasha kutumika.

Alisema kuwa kuwa kulikuwa na taarifa za awali kuwa kungekuwa na kikao cha wafanyakazi yote kiwandani hayo na uongozi wa kiwanda, na kuwa taarifa hizo ziribadilishwa Januari 23 siku tatu kabla ya tukio na wafanyakazi walio kuwa wamekuja asuhi siku ya tukio walikuwa hawana taarifa za mabadiliko ya mkutano huo.

Alisema kuwa alisema kuwa wafanyakazia hao hawakuja kiwandani hapo asubuki kwa lengo la kufanya mgomo lakini kulikuwa na mkanganyiko wa taarifa za kikao hicho, na kuwa kitendo kilicho fanywa na jeshi la polisi hakikuwa sahihi.
   
Alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wamepigwa walikuwa wamekuja kiwandani hapo ulikuwa ni mda wao wa kazi, na wengine walikuja hapo wakiwa na taarifa za mkutano wa saa 3 asubuhi, alisema baada ya kuzungumza na uongozi ulisema kuwa uliita polisi baada ya kuona baadhi ya matangazo ya mkutano kuwa yameondolewa.

Kitendo hiki kinatakiwa kupingwa na jamii yote na jeshi la pilisi sio sehemu ya kutatua matatizo ya wafanyakazi na kuwa kwa mujibu wa sheria ya wafanyakazi Polisi watahusika poale tu patakapo kuwa na uvunjifu wa amani mahara pa kazi lakini kiwandani hapa hapakuw ana uvunjifu wa amani.

“Polisi watahusika pale tu patakapo kuwa na uvunjifu wa amani, lakini wafanyakazi walikuwa nje ya geti walikuwa wamekaa kwa hiyo kulikuwa na amani polisi wamewapiga wafanyakazi na wengine walikuwa wamelala, na wengine kuibiwa pesa na mfanyakazi huyo ameeleza mbele ya uongozi amechukuliwa shilingi laki 3 (300,000) ambazo anafanyia biashara ya M-pesa na mwingine amepigwa akiwa uchi wakati akibadilisha nguo wamemfuata nyumbani kwake,” alisema Magesa.

Alisema kuwa wamekaa na uongozi wa kiwanda kikao ambacho kimedumu kwa zaidi ya masaa manne ambapo anamesema kuwa walizungumza na uongozi wa kiwanda na kuwa wamefikia maamuzi ya kuwa mkutano baina ya uongozi na wafanyakazi utakuwa Februari 23, na uongozi umekubali kuwa waliwaita polisi lakini hawakuwataka watumie nguvu waliyo itumia.

“Uongozi tulipo uuliza kwanini ulitumia guvu hiyo ulisema kuwa haukuliambia jeshi hilo litumie nguvu hiyo na kuwa uongozi unashanga kwa kilew kilichotokea, tumeutaka uongozi kuwaachia wale walio shikiliwa na jeshi la Polisi na wataendelea na kazi hadi watakapo kaa kikao chao na wale walio pata madhara tutaibana menejimenti kuhakikisha inawafidia,” aliongeza Magesa.

Waandishi wa hanari walifika katika ofisi ya uongozi wa kiwanda hicho kutaka kujua mengi zaidi kuhusiana na kilichotokea na maamuzi waliyo yafikia lakini meneja wa kiwanda hicho Miraji Gembe alisema kuwa hayupo tayari kuzungumza chohote kwa kuwa anashughulika na watu wa usalama (Polisi).

Kwa upande wake kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Lucy Mwakafywila alisema kuwa wanawashikilia  wafanyakazi 14  wa kiwanda cha chai wanashikiliwa kufuatia tatizo  hilo kwaajili ya uchunguzi  huku  wafanyakazi 26  waliokamatwa juzi wakiachiwa. 


Kamanda Mwakafulila alisema kuwa polisi  walilazimika kutumia mabomu ya machozi  kwa lengo la kuwatawanya wafanyakazi ambao hawakupaswa kuingia kazini  ambapo anasema kwa taarifa silizo mfikia hakuna mtu yaliye pigwa tofauti na kile Elimtaa ilichojionea katika eneo la tukio.



Aidha alisema kuwa jeshi la polisi lilipangwa kuimarisha ulinzi na usalama  kwenye kiwanda na siyo kwenda kwenye  kambi za kiwanda hicho kama wanavyolalamikia wafanyakazi hao  kwamba jeshi hilo lilikwenda kabini kuwavunjia milango na kuwapiga na virungu na wengine wakidaiwa kuibiwa simu na fedha zao