Fidel Odinga mwana wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amepatikana akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen.
Maafisa wa polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mfanyibiashara huyo ambaye pia amekuwa akionekana katika ulingo wa kisiasa.
Maafisa wa Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa mapema umeonyesha kuwa Fidel alikuwa nje usiku wa jumamosi na alirudi mapema jumapili.
Haijulikani ni nini kilichosababisha kifo chake.
Kundi la wabunge pamoja na maseneta liliwasili katika nyumba ya Raila baada ya kupata habari hizo.
Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa jumamosi na alikuwa na nani.