Jeshi nchini Burundi linasema kuwa watu kadha wameuawa kwenye mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.
Karibu waasi 200 wanaripotiwa kuvuka na kuingia eneo lililo kaskazini magharibi mwa Burundi kutoka jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na kuzua mapigano yaliyodumu kwa siku kadhaa.
Jeshi nchini Burundi linasema kuwa wengi wa wale walilokufa ni waasi na kwamba silaha nyingi zimepatikana.
Hadi sasa haijulikani waasi hao ni kutoka kundi gani.
Mashambulizi ya hapo awali katika eneo hilo yamekuwa yakitekelezwa kundi lililojitenga la FNL ambalo liliingia katika mktaba wa amani na serikali mwaka 2009.