MAKAMANDA WOTE WA UKAWA TANZANIA ILI KUIPELEKA CCM KUZIMU KILA MKOA TUFANYE HIVI;


Ninaamini Ukawa inaweza kushinda iwapo kampeni na mikakati itawekwa kulingana na mchanganuo ufuatao.Hii ni sayansi sio porojo...
1.Arusha ina majimbo 7 Ukawa wanatakiwa kuchukua majimbo manne tu.yaani kuongeza jimbo la Arumeru Magharibi.
2.Dodoma ina majimbo 9 Ukawa inatakiwa kunyakua mawili tu.huku bado watu hawajaelimika sana.
3.Kilimanjaro ina Majimbo 9 Ukawa wanatakiwa kuchukua majimbo sita.vunjo na Siha ni lazima yakombolewe.
4.Tanga ina majimbo 11 na pia kuna idadi kubwa ya wapiga kura.UKAWA kupitia CUF wachukue angalau majimbo mawili.
5.Morogoro kuna majimbo 10 lakini idadi ya wapiga kura inaendana na Tanga.hapa Ukawa wachukue majimbo manne.Kilosa,mvomero,moro mjini,Ifakara.
6.Pwani ina majimbo tisa lakini wapiga kura ni wachache.hapa ukawa ichukue majimbo mawili tu.Chalinze au bagamoyo na kibaha.
7.Daresalaam ina majimbo saba lakini wapiga kura ni wengi.hapa Ukawa ichukue majimbo matano.Ilala,Temeke,Ubungo,Seg erea na kigamboni.
8.Lindi ina majimbo nane na wapiga kura ni wachache.hapa Ukawa kupitia Cuf ichukue matano tu.
9.Mtwara ina majimbo 7 wapiga kura wanakaribiana na Lindi.hapa Ukawa ichukue manne.
10.Ruvuma ina majimbo 6 Ukawa wachukue matatu tu.
11.Iringa ina majimbo 11 na wapiga kura ni karibu ya milioni.hapa Ukawa ichukue matano.
12.mbeya ina majimbo 11 hapa Ukawa ipambane na kuchukua sita.wapiga kura ni zaidi ya milioni moja.mbeya mjini isiachwe.
13.Singida kuna majimbo saba ukawa ichukue matatu tu.cuf mawili na chadema moja.
14.Tabora ina majimbo 9 lakini wapiga kura ni zaidi ya milioni moja.Ukawa ichukue majimbo manne.moja kwa chadema na mengine kwa Cuf.Tabora imetengwa sana katika harakati za ukawa lakini ni kitovu muhimu cha mapambano.
15.Rukwa ina majimbo 7 lakini idadi ya wapiga kura yaweza lingana na Arusha...laki saba na ushee.hapa ukawa wachukue matatu tu.
16.Kigoma ina majimbo 7 na idadi ya wapiga kura inarandana na rukwa au arusha.ukawa wachukue majimbo 6 na moja laweza kwenda ACT.lakini kwa kesi ya urais ccm hawataambulia kitu.
17.Shinyanga ina majimbo 11 na idadi ya wapiga kura ni kubwa ...ni zaidi ya milioni moja na nusu.hapa ukawa ni lazima wanyakuwe majimbo 7.
18.Kagera ina majimbo kumi na idadi ya wapiga kura ni zaidi ya milioni moja.ukawa igawane majimbo na kujihakikishia matano tu.muleba yote isiachwe!
19.Mwanza ina majimbo 13 na wapiga kura zaidi ya milioni moja na laki sita.hapa ndio mtanange kwani ukawa lazima ijinyakulie majimbo 8 ili kujihakikishia ushindi.
20.Mara ina majimbo 7 Ukawa inatakiwa kuchukua matano kama Arusha.
21.Manyara ina majimbo sita lakini wapiga kura ni wachache kama laki sita hivi.ukawa ichukue matatu tu ...simanjiro na kule kwa Nagu.
UKAWA ikifanikiwa kuwekeza kwa formula hii ccm itabaki historia na nchi itaendeshwa kwa maamuzi safi bungeni. Pia kama kila anayempigia mbunge wa UKAWA atampigia na mgombea urais wa UKAWA, basi hata urais CCM kifo cha mende kabisa...!
Hapa imewekwa assumption ya kuwa majimbo hayatabadilishwa na kura za zanzibar hazitaathiri matokeo kwani kile ni nusu kwa nusu.
INAWEZEKANA, KILA MTU ATIMIZE JUKUMU LAKE.