Korea Kazkazini yaionya Marekani

  • Saa 9 zilizopita
Rais Obama wa marekani na rais kim jon un wa korea kazkazini
Korea kazkazini imeonya kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi yake ni kitendo cha uadui ambacho hakitafanikiwa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni amenukuliwa na vyombo vya habari vya serikali akisema kuwa vikwazo hivyo vitaifanya korea kaskazini kuwa mbaya zaidi ili kulinda uhuru wake.
Rais Obama aliiwekea korea kaskazini vikwazo siku ya Ijumaa akiishutumu kwa kundesha uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures ilipokuwa ikijiandaa kuonyesha filamu ya dhihaka ya kuuawa wa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong-un.