Diwani huyo amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupita katika ofisi za CCM wilaya akitokea kwenye ofisi za afya za manispaa ya Shinyanga zilizopo jirani na jengo hilo la CCM,ambapo ghafla vijana hao waliokuwa wamefunga ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakishinikiza viongozi wa ngazi ya wilaya waondolewe madarakani kutokana na kuonekana kusaliti CCM na kufanya ishindwe katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika manispaa ya Shinyanga walipomvamia na kuanza kumshambulia wakidai hawataki viongozi wa upinzani wapite hapo kwani huwa wanaiba siri za CCM-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Diwani wa CHADEMA George Sungura akisukumwa barabarani -picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
|
Diwani wa Kata ya Ndala George Sungura akizungumza katika moja ya mikutano ya CHADEMA mwaka 2014-Picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog.Kufuatia tukio hilo diwani huyo amesema anafungua kesi polisi kutokana na kitendo hicho cha kudhalilishwa mbele ya umma.Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Tajiri Maulid amesema CCM itawachukulia hatua za kidhamu vijana hao