Maambukizi ya Ebola yaongezeka Sierra Leone

Idadi  ya  watu  walioambukizwa  na  ugonjwa  wa  Ebola  kaskazini mwa  Sierra  Leone , upande mwingine  wa  nchi  hiyo  ambako maambukizi  ya  kwanza  yalijitokeza  miezi kadhaa  iliyopita, inaongezeka ambako  kumekuwa  na  vifo  vya  watu 20  kila  siku. Maambukizi  mapya  ya  Ebola  yaliyothibitishwa  hadi  jana Jumatatu  katika  kanda  yenye  ugonjwa  wa  Ebola  nje  na  ndani ya  mji  mkuu Freetown  imefikia  49. Kituo  cha taifa  cha kupambana  na  ugonjwa  wa  Ebola  kimeripoti  leo, kuwa  kuna jumla  ya  watu  851  waliothibika  kuwa  na  ugonjwa  huo  katika kanda  hizo  mbili, ambazo  ni  eneo  la  magharibi  ya  mji  na  eneo la  magharibi  la  vijijini. Lakini  hakuna  maambukizi  mapya  katika eneo  la  wilaya  za  mashariki  za  Kenema  na  Kailahun, ambazo hapo  kabla  zilikuwa eneo lililozuka  ugonjwa  huo na  ambapo  kuna watu  zaidi  ya  1,012  ambao  wamethibika  kuwa  na  ugonjwa  huo.
Wakati  huo  huo chombo  kimya kitawaruhusu  madaktari kumchunguza  mgonjwa anayeshukiwa  kuwa  na  virusi  vya  Ebola katika  muda  wa  dakika  15, na  chombo  hicho kinaweza kupatikana  katika  nchi zilizoathirika  na  ugonjwa  huo ifikapo mwishoni  mwa  Oktoba.